UINGEREZA-UHISPANIA-UJERUMANI-ITALIA - 
Makala iliyochapishwa tarehe : Thursday 20 septemba 2012 - Taarifa za ivi karibuni : Thursday 20 septemba 2012

Manchester United na Barcelona washinda huku Bingwa Mtetezi Chelsea akibanwa mbavu nyumbani

Kiungo wa Kimataifa wa Uingereza na Klabu ya Manchester United Michael Carrick akishangilia goli lake na Robin Van Persie
Kiungo wa Kimataifa wa Uingereza na Klabu ya Manchester United Michael Carrick akishangilia goli lake na Robin Van Persie

Na Nurdin Selemani Ramadhani

Goli la mapema lililofungwa na Kiungo wa kimataifa wa Uingereza anayekipiga na klabu ya Manchester United lilitisha kuwapa ushindi mwembamba timu hiyo kwenye mchezo wao wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya mbele ya Galatasary.

Ushindi huo ulikuwa ni wa mia moja kwa Kocha Mkuu wa Manchester United Sir Alex Ferguson ambaye alishuhudia kiungo wake Luis Nani akikosa mkwaju wa penalty na washambuliaji wake wakipoteza nafasi nyingi ambazo walizipata.

Mabingwa watetezi Chelsea walianza kwa sare ya magoli 2-2 mashindano ya mwaka huu mbele ya Juventus ambao walikuwa wageni kwenye uwanja wa Stamford Bridge na kushuhudia wenyeji wakiongoza kwa magoli mawili.

Kinda Mbrazil Oscar ndiye ambaye aliifungia Chelsea magoli yote mawili kabla ya Juventus kuja juu na kusawazisha kupitia Arturo Vidal kabla ya mchezaji aliyeingia kipindi cha pili Fabio Quagliarella kufunga goli la pili.

FC Barcelona wakiwa nyumbani Nou Camp walifanikiwa kuchomoza na ushindi wa magoli mawili dhidi ya Spartak Moscow ambayo iliweza kuongoza lakini ikajikuta hadi mwisho inakumbana na kichapo cha magoli 3-2.

Lionel Messi alifunga magoli mawili kuisaidia klabu yake kupata ushindi wa nyumbani baada ya kinda Cristian Tello kufunga goli la kwanza huku Spartak Moscow wakipata magoli yao kupitia Dani Alves na Romulo.

Bayern Munich wakiwa nyumbani wakafanikiwa kuwafunga Valencia kwa magoli mawili kwa 2-1 kupitia kwa Bastian Schweinsteiger na Toni Kroos wakati wapinzani wao wakipata goli lao lilofungwa na Nelson Valdez.

Lille ikiwa nyumbani Ufaransa ikapata kichapo kizito cha magoli 3-1 kutoka kwa wageni wao BATE Borisov huku Celtic wakienda suluhu tasa na Benfica mchezo ambao umepingwa nchini Scotland.

tags: Alex Ferguson - Chelsea - FC Barcelona - Juventus - Manchester United
MAELEZO
Tuma maoni yako kwa makala haya
Maudhui ya eneo hili yatakuwa ya kibinafsi na kuto kuonyeshwa kwa watu wote.
To prevent automated spam submissions leave this field empty.
CAPTCHA
Swali hili ni kwa ajili ya kupima kama wewe si roboti ili kuzuia spam ya papo kwa papo.
Close