Pata taarifa kuu
LiGI KUU YA ULAYA-UEFA

Bayern Munich na Atletico Madrid zafuzu nusu fainali ya michuano ya UEFA.

Klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani, na Athetico Madrid ya Uhispania zimejiunga na Chelsea ya Uingereza, na Real Madrid ya Uhispania katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya kuwania taji la klabu bingwa barani Ulaya msimu huu.

Bayern Munich wafuzu baada ya kuwafunga Manchester United mabao 3-1 katika mchuano wa marudiano katika uwanja wao wa nyumbani wa Allianze Arena.
Bayern Munich wafuzu baada ya kuwafunga Manchester United mabao 3-1 katika mchuano wa marudiano katika uwanja wao wa nyumbani wa Allianze Arena. REUTERS/Stefan Wermuth
Matangazo ya kibiashara

Bayern Munich wamefuzu baada ya kuwafunga Manchester United ya Uingereza mabao 3 kwa 1 katika mchuano wa marudiano katika uwanja wao wa nyumbani wa Allianze Arena.

Mabao ya munich ambao pia ni mabingwa watetezi yalitiwa kimyani na Mario Mandzukic, Thomas Muller na Arjen Robben katika kipindi cha mchuano huo, huku bao la United likitiwa kimyani mwanzoni mwa kipindi cha pili kupitia mchezaji Patrice Evra kabla ya Munich kusawazisha na kupata ushindi.

Matumaini ya Manchester United kuwatuliza mashabiki wake, kwa kufanya vizuri katika michuano hii ya UEFA yameisha baada ya kupoteza, na huu utasalia msimu mgumu kwa vijana wa David Moyes ambao walicheza kwa kulinda golo lao katika mchuano wa jana.

Nao mabingwa wa zamani, Barcelona ya Uhispania licha ya kutawala mchezo wa jana usiku wamebanduliwa nje ya michunao hiyo na ndugu zao Athletico Madrid pia kutoka Uhispania kwa kufungwa bao 1 kwa 0 na kufuzu kwa jumla ya mabao 2 kwa 1 baada ya kutoaka sare ya bao 1 kwa 1 katika mchuano wa mzunguko wa kwanza.

Athletico Madrid ilipata bao hilo katika dakika ya tano ya mchezo huo kupitia kwa kiungo wa kati wa Jorge Resurreccion alimaarufu kama Koke, na kuifikisha klabu hiyo katika hatua hiyo ya nusu fainali kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1974.

Barcelona imeshindwa kufika katika hatua ya nusu fainali ya michuano hii kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2007.

Droo ya michuano ya nusu fainali itafanyika tarehe 11 mwezi huu na michuano ya mzunguko wa kwanza itachezwa tarehe 22 na tarehe 23.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.