Pata taarifa kuu
RATIBA KLABU BINGWA ULAYA

Chelsea mdomoni mwa Atletico Madrid nusu fainali ligi ya mabingwa Ulaya

Hatimaye ratiba ya michuano ya nusu fainali ya klabu bingwa Ulaya na ile ya Europa imetangazwa na shirikisho la kabumbu barani Ulaya UEFA, huku mabingwa watetezi klabu ya Beyern Munich ikipangiwa kucheza na Real Madrid ya Uhispania.

UEFA.com
Matangazo ya kibiashara

Ratiba hiyo imetolewa siku ya Ijumaa ya tarehe 11 mwezi April kwenye makao makuu ya shirikisho la mpira la Ulaya UEFA ambapo kiu ya mashabiki sasa itakuwa imekatwa kwakuwa wengi walikuwa wakisubiri kuona ratiba hiyo.

PICHA ZA TIMU

Klabu ya Uingereza ya Chelsea maarufu kama The Blues yenyewe itasafiri hadi mjini Madrid nchini Uhispania kuwakabili Atletico Madrid ambao wanaongoza kwenye ligi yao ya nyumbani.

Chelsea inaingia kwenye mchezo huu wa nusu fainali ikisaka nafasi ya kushiriki kwa mara ya tatu katika fainali ya michuano hiyo kwa msimu wa saba mfululizo, safari hii ikiwa chini ya Kocha Josee Mourinho.

Nusu fainali ya kwanza itapigwa tarehe 22 ya mwezi wa 4 mwaka huu.

Nusu fainali nyingine kwenye michuano hiyo itawakutanisha mabingwa watetezi wa kombe hili, klabu ya Ujerumani, FC Beyern Munich ambayo baada ya kuitupa nje ya michuano hii klabu ya Manchester United, sasa itasafiri hadi katika uwanja wa Santiago Bernabeu kuwakabili klabu ya Real Madrid ya Uhispania.

Kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti anatakiwa kushinda kwenye mechi zote mbili iwapo anataka kutwaa kombe hili kwa mara ya kumi na klabu ya Real Madrid, jambo ambalo wachambuzi wa mambo wanaona kuwa linawezekana kutokana na umahiri wa timu zote mbili.

Katika michuano ya kombe la Europa, klabu ya Benfica ya nchini Ureno yenyewe imepangwa kucheza hatua ya nusu fainali na klabu ya Italia ya Juventus ambao wanapewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa huo mwaka huu.

Sevilla ya Uhispania yenyewe itabaki nyumbani kuwakaribisha majirani zake pia wa Uhispania klabu ya Valencia kwenye mchezo mwingine ambao unatarajiwa kuwa wa upinzani kwakuwa unahusisha timu mbili zinazocheza ligi moja ya Uhispania.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.