Pata taarifa kuu
KOMBE LA DUNIA BRAZIL 2014

Wasifu wa Timu ya Taifa ya australia

Imeshiriki mara 3, haijawahi kushinda taji hili, iko katika nafasi ya 59 kwenye viwango vya FIFA.Historia kwenye kombe la dunia la FIFA.“ The Socceroos” kama inavyojulikana, Imeshiriki fainali za kombe la dunia za mwaka 1974 zilizofanyika nchini Chile na kumaliza michuano hiyo bila hata kufunga goli moja kwa kile wachambuzi wanasema timu hii inaundwa na wachezaji wengi wanaocheza ligi za ndani. Licha ya kushiriki mara tatu kwenye michuano hii, Australia haijwahi kufanya vizuri zaidi ya kupoteza mechi zote inazocheza. 

Timu ya Taifa ya Australia
Timu ya Taifa ya Australia fifa.com
Matangazo ya kibiashara

Kundi ililopo.

Timu ya taifa ya Austalia iko kwenye kundi B la michuano ya mwaka huu ikiwa ni pamoja na timu za taifa za Uhispania, Uholanzi na Chile.

Wachezaji wakuangaliwa.

Mchezaji pekee anayetajwa kuwa huenda akaisaidia sana timu yake kutokana na uzoefu alionao kwenye ligi kuu ya Uingereza ni mchezaji, Tim Cahill. Wengine wanaotazamiwa kuleta chachu ya ushindani kwa timu hii ni pamoja na Lucas Neill.

Benchi la Ufundi.

Timu ya taifa ya Australia inaongozwa na kocha mkuu, Ange Postecoglou.

Wachezaji waliovuma.

Ni pamoja na Johnny Warren, Mark Viduka na Scott Chipperfield.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.