Pata taarifa kuu
KOMBE LA DUNIA BRAZIL 2014

Wasifu wa Timu ya Taifa ya Ugiriki

Imeshiriki mara 2, haijawahi kushinda taji hili, iko katika nafasi ya 10 kwenye viwango vya FIFA.Historia kwenye kombe la dunia la FIFA.“To Piratiko” ama meli ya maharamia kama wanavyofahamika, Ugiriki inajivunia historia nzuri ya michuano ya kombe la Ulaya ya mwaka 2004 nchini Ureno. Mwaka 1994 kwenye fainali za kombe la dunia nchini Marekani ilirejea nyumbani bila ya alama yoyote lakini licha ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Nigeria na kupoteza dhidi ya Korea kwa mabao 2-0 kwenye fainali ya Afrika Kusini bado timu hii imeshindwa kufanya vema. 

Timu ya Taifa ya Ugiriki
Timu ya Taifa ya Ugiriki fifa.com
Matangazo ya kibiashara

Kundi ililopo.

Ugiriki iko kwenye kundi C ikijumuishwa na timu za Colombia, Ivory Coast na Japan, hili linatajwa kutokuwa kundi gumu sana kwenye michuano ya mwaka huu.

Wachezaji wakuangaliwa.

Miongoni mwa wachezaji wanaotarajiwa kuwa chachu ya ushindi wa timu ya taifa ya Ugiriki ni pamoja na Giorgos Karagounis, Dimitrioa Salpingidis, Theofanis Gekas na Giorgos Samaras ni miongoni mwa wachezaji ambao wanatazamwa kuwa na mchango mkubwa kwenye timu.

Benchi la Ufundi.

Timu ya taifa ya Ugiriki inaongozwa na kocha mkuu, Fernando Santos.

Historia pekee kwenye michuano ya kombe la dunia la FIFA.

Ni ushiriki wake wa kombe la dunia mwaka 1994 na kule Afrika Kusini ambapo ilimaliza kwenye hatua ya makundi.

Wachezaji wanaovuma.

Ni pamoja na Theodoros Zagorakis, Antonios Nikopolidis na Angelos Basinas.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.