Boston: Mamia ya wanariadha wajitokeza kushiriki mbio za marathon
Takriban watu milioni moja na wanariadha elfu 35, wanasubiriwa leo jijini Boston nchini Marekani kuadhimisha mbio za Marathon ikiwa ni mwaka mmoja tangu kutokea kwa mlipuko wa bomu uliogharimu maisha ya watu watatu, na ambapo mwaka huu polisi imetanda katika kila kona kuhakikisha usalama umaimarika.
Imechapishwa:
Polisi wapatao elfu tatu na mia tano wametawanywa katika mji mkuu wa Massachusetts kaskazini mashariki mwa Marekani ikiwa ni mara mbili ya idadi iliokuwa mwaka uliopita, zaidi ya hao walinzi wa kikosi cha taifa wapata 600 na wengine walinzi 3.500 wa kampuni binafsi.
Kamati ya maandalizi ya mbio hizo imedhamiria usalama vya kutosha wakati huu idadi pia ya wanariadha ikiongezeka, ukilinganisha na mwaka uliopita. Mbio hizo zliingia dosari mwaka jana pale vijana wawili wa kiislam wenye asili ya ki tchetcheni walitega bomu ndani ya begi lililolipuka na kugharimu maisha ya watu watatu.
Kamati ya maandalizi imechukua hatua zinazohakikisha kuwa usalama umeimarishwa ipasavyo, huku mifuko yoyote ikipigwa marufuku, na kuamrisha watakaohudhuruia mbiyo hizo iwapo watapendelea kutumia mifuko ya kuhifadhi nguo zao watumiye mifuko inayoonshesha kilicho ndani.
Bomu liliyolipuka mwaka jana liliwekwa ndani ya mfuko unaobebwa mgongoni na baadae uliwekwa kwenye aridhi na ndugu wawili kutoka jamii ya waislamu raia wa Checheniya.
“Tuko makaini , na tumejiandalia vizuri. Tunawapa matumaini watu wanaoshiriki na wale wanaohudhuria mbio hizi kwamba leo ni sikukuu kubwa, na siku ya matumaini”, mkuu wa jimbo la Deval Patrick, ameelezea jana jumapili, kituocha habari cha CBS.
Kwa mujibu wa kamati ya maadalizi, zaidi ya wanahabari 1800 wamejielekeza mjini Boston kuhudhuria mbio hizo.
Vijana waliyohusika katika shambulio la bomu mjini Boston, mmoja, ambaye anajulikana kwa jina la Djokhar, mwenye umri wa miaka 19 yu hai na mwengine, Tamerlan Tsarnaev, mwenye umri wa miaka 26 aliuawa na polisi alipokua akijaribu kujificha, aprili 19 mwaka jana. Picha ya mtuhumiwa huyo aliyeuawa hii hapa.
Djokhar, anakabiliwa na adhabu ya kifo, na hukumu yake itatolewa novemba 3 mwaka huu.