Pata taarifa kuu
SOKA BARANI ULAYA

Antoine Grizmann ajiunga na klabu ya Atletico Madrid

Atletico Madrid na Real Sociedad wamefikia mkataba wa kumuuza mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa, Antoine Griezmann, ambaye kwa sasa ataichezea klabu ya Atletico Madrid, imethibitisha klabu hiyo.

Antoine Griezmann (kusoto) akikabiliana na Sami Khedira.
Antoine Griezmann (kusoto) akikabiliana na Sami Khedira. REUTERS/Darren Staples
Matangazo ya kibiashara

Mchezaji huyo ambaye bado kijana mdogo, alizaliwa mwaka 1991, katika mtaa ulioko mkatikati ya Ufaransa, atafanyiwa uchunguzi wa afya, kabla ya kusaini mkataba wake, Atletico Madrid, imethibitisha katika mtandao wake wa intaneti.

Klabu ya Real Sociedad imempongeza Antoine Griezmann kwa ushiriki aliyotoa kwa klabu hiyo tangu alipojiunga nayo.

Real Sociedad imebaini kwamba Antoine Griezmann ni kiungo tosha, ambaye alijiunga na klabu hiyo akiwa na umri wa miaka 13, na alianza kuichezea mwaka 2009.

Griezmann ameshiriki mechi 202 akiichezea klabu ya Real Sociedad, huku akiweka wavuni mabao 53, imeendelea kusema Real Sociedad.

Hayo yakijiri, wiki mbili baada ya kumalizika kwa michuano ya kombe iliyochezwa nchini Brazil, timu za daraja la kwanza nchini Ufaransa zinajipanga kumenyana, huku mechi ya ufunguzi ikiwa inatarajiwa kuchezwa mnamo siku 12 zijazo kati ya Reims na PSG.

Wachezaji wa kikosi cha klabu ya PSG ikiwa ni pamoja na Lucas(kusoto), Alex (katikati) na Maxwel (kulia)l.
Wachezaji wa kikosi cha klabu ya PSG ikiwa ni pamoja na Lucas(kusoto), Alex (katikati) na Maxwel (kulia)l.

Michuano ya kombe la dunia ilimalizika Julai 13 nchini Brazil, ikiwa iliwachia simanzi kubwa wachezaji wawili raia wa Argentina, baada ya timu yao kufungwa na Ujerumani katika fainali. Wachezaji hao ambao pia ni wachezaji bora wa timu za daraja ya kwanza ya Ufaransa ni Lavezzi ambae anaichezea PSG, na Romero anayeichezea Monaco.

Wachezaji wengine wa PSG waliyopata zimanzi kutokana na michuano hiyo ya kombe la dunia ni Thiago Silva, David Luiz na Maxwell (wote raia wa Brazil), ambao hawataonekana uwanjani Ogasti 8 katika mechi ya PSG na Reims, baada ya kuomba likizo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.