Pata taarifa kuu
SOKA BARANI ULAYA

Angel Di Maria avunja rekodi Uingereza

Kununuliwa kwa mchezaji wa kimataifa Angel Di Maria kutoka klabu ya Real Madrid na kujiunga na klabu ya Manchester United kwa muda wa miaka 5 imekua ni gumzo kwa jamii ya wanasoka ulimwenguni.

Angel Di Maria anunuliwa na Manchester United kwa kitita Uro cha milioni 75.
Angel Di Maria anunuliwa na Manchester United kwa kitita Uro cha milioni 75. REUTERS/Ivan Alvarado
Matangazo ya kibiashara

Mwaka huu pekee, kabla ya Angel Di Maria, walinunuliwa wachezaji wa kimataifa kutoka vilabu mbalimbali barani Ulaya, hususan Luis suarez ambaye alinunukiwa na Barcelona akitokea Liverpool, David Luiz baada ya kuichezea Chelsea alijiunga na Paris saint Germain, huku James Rodriguez akijiunga na Real Madrid akitokea Monaco.

Di Maria ni mchezaji wa tatu, kununuliwa kwa kitita kikubwa cha Uro milioni 75, baada ya Cristiano Ronaldo kununuliwa na Real Madrid akitokea manchester United kwa kitita cha Uro milioni 94, naye Gareth Bale akitokea Juventus alinunuliwa na Real Madrid kwa kitita cha Uro milioni 91. Di Maria amenunuliwa kwa kiwango alichonunuliwa Zinédine Zidane kutoka Tottenham kujiunga na Real. Mwaka 2011, Fernando Torres alinunuliwa na Chelsea kaitokea Liverpool kwa kitita cha Uro milioni 60.

DI maria haja amevunja rekodi ya Uingereza, lakini ya dunia bado inashikiliwa na Cristiano Ronaldo.

Di Mari, raia wa Argentina, mwenye umri wa miaka 26, alianza na timu ya nyumbani kwao ya Rosario Central, na alianza kujizolea umaarufu mwaka 2007-2010 alipokua akiichezea Benfika, kabla ya kujiunga na Real Madrid, ambapo kila msimu alikua akifunga.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.