Pata taarifa kuu
FIFA-UEFA-Uchaguzi

Michel Platini abadili niya yake ya kugombea kwenye kiti cha urais wa Fifa

Michel Platini, ambaye ni rais wa shirikisho la soka barani Ulaya UEFA, ametangaza kwamba hatogombea katika uchaguzi wa urais wa shirikisho la soka duniani Fifa.

Rais wa shirikisho la soka la Ulaya UEFA, Michel Platini.
Rais wa shirikisho la soka la Ulaya UEFA, Michel Platini. Reuters
Matangazo ya kibiashara

“Ni chaguo langu, ambalo limetoka moyoni, nitagombea katika muhula mpya wa shirikisho la soka barani Ulaya, wala siyo Fifa, huo ndiyo uamzi wangu”, amesema nahodha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa mele ya vyombo vya habari vya kimataifa mjini Monaco.

Akihojiwa kuhusu kugombea kwenye kiti cha urais wa Fifa, Platini, amesema muda haujawadia.
“muda wa kugombea kugombea kwenye kiti cha urais wa Fifa haujawadia, bado natafakari, lakini bado sijaona umuhimu”, amesema Platini.

Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Mei 29 mwaka 2015 mjini Zurich. Jérôme Champagne, mwenye umri wa miaka 56 sawa na Michel Platini, ambaye ni katibu mkuu wa Fifa atagombea kwenye kiti cha urais wa Fifa, naye rais wa sasa wa shirikisho hilo, Joseph Blatter, mwenye umri wa miaka 78, akiwa kwenye wadhifa huo tangu mwaka 1998, amesema yuko tayari kugombea kwa muhula wa tano.

Champagne, mwanadiplomasia wa zamani wa Ufaransa, anaonekana kutokua na nafasi nzuri ya kupigiwa kura, baada ya mwenyewe kuthibitisha kwamba haamini iwapo atapigiwa kura iwapo Blatter atagombea.

Rais wa sasa waFIFA, Joseph Blatter.
Rais wa sasa waFIFA, Joseph Blatter. Reuters

Blatter bado hajaonesha niya yake ya kugombea kwenye kiti hicho,lakini katika kikao cha Fifa kiliyofanyika Sao Palo mwanzoni mwa Juni, raia huyo wa Uswisi alieleza wajumbe walioshiriki kikao hicho kwamba yuko tayari kushirikiana nao katika miaka ijayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.