Pata taarifa kuu
Michezo - klabu bingwa Africa

TP Mazembe washindwa kutamba nyumbani na waenguliwa kwenye fainali za michuano ya klabu bingwa

Klabu ya soka ya TP Mazembe imeshindwa kufuzu katika hatua ya fainali ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika licha ya kuifunga Es Setif ya Tunisia mabao 3 kwa 2 jioni hii mjini Lumbumbashi katika mchuano wa pili wa nusu fainali.

KLABU YA TP Mazembe
KLABU YA TP Mazembe tp mazembe
Matangazo ya kibiashara

Mazembe ambao wamewahi kushinda taji hili mara nne wameshindwa kusonga mbele kutokana na ushindi wa Setif wa mabao 2 kwa 1 juma lililopita.

Sasa mataumi ya mashabiki wa soka nchini DRC yamesalia kwa klabu ya Vita Club yenye makao yake jijini Kinsasha ambayo iliweka hitoria jana kufuzu fainali kwa Kuifunga CS Sfaxien ya Tunisia mabao 2 kwa 1 ugenini kama ilivyofanya nyumbani wiki iliyopita.

Vita club inakuwa klabu ya kwanza klatika historia ya michuano ya CAF kupata ushindi katika hatua ya nusu fainali nyumbani na ugenini kwa kuifunga timu pinzani kwa mabao 2 kwa 1.

Vita Club sasa itamenyana na ES Setif ya Tunisia katika hatua ya fainali kuanzia mwezi ujao na mshindi kuliwakilisha bara la Afrika katika michuano ya klabu bingwa duniani nchini Morroco mwezi Desemba
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.