Nigeria: Meneja wa timu ya taifa ya Nigeria afutwa kazi
Shirikisho la soka nchini Nigeria limemfuta kazi, kocha wa timu ya taifa Stephen Keshi licha ya ushindi wa Super Eagles dhidi ya Sudan.
Imechapishwa:
Nigeria imeibwagiza Sudan mabao 3 kwa 1 jana Jumatano jijini Abuja katika mchuano wa kusakata tiketi ya kufuzu kwa michuano ya kuwania ubingwa wa Afrika mwaka ujao nchini Morroco mwaka ujao.
Kocha wa zamani Shuaibu Amodu amepewa kazi ya kuifunza Nigeria kwa muda mfupi kabla ya kuajiriwa kwa kocha mwingine kutoka nchi ya kigeni.
Amodu ataingoza Nigeria katika michuano inayosalia ya kutafuta tiketi ya kwenda Morroco baada ya ushindi wa Jumatano wiki hii, ambapo Super Eagles wanahitaji kushinda mechi zinazosalia.
Kwa sasa Nigeria wana alama nne katika kundi la A, na ushindi wa jana ulikuwa wa kwanza tangu kuanza kwa kampeni hii.
Wachambuzi wa soka wanasema ilitarajiwa Keshi kufutwa kazi baada ya kuingoza Nigeria katika kombe la dunia nchini Brazil mwaka huu, na pia kuisaidia Super Eagles kunyakua taji la Afrika mwaka jana, na kutofanya vizuri katika michuano ya kwenda Morroco.
Viongozi wa kandanda nchini Nigeria wamesema wamechukua hatua hiyo kwa maslahi ya mchezo huo nchini humo, na kumpa Keshi nafasi ya kumpumzika baada ya kuisaidia Super Eagles.
Keshi mwenye umri wa miaka 52 aliteulwia kuifunza Super Eagles mwaka 2011, na pia aliwahi kuwa kocha wa timu ya taifa ya Togo na Mali kati ya mwaka 2004 na 2011.