Pata taarifa kuu
AFRIKA-SOKA-MICHEZO-MOROCCO-CAN 2015

CAN 2015: Ebola: Morocco yakanusha tuhuma dhidi yake

Serikali ya Morroco imekanusha madai kuwa inapanga kujiondoa kuwa mwenyeji wa michuano ya soka kuwania taji la mataifa bingwa barani Afrika mapema mwaka ujao kutokana na hofu ya kusambaa kwa ugonjwa hatari wa Ebola.

Morocco yakanusha madai kuwa inapanga kujiondoa kuwa mwenyeji wa michuano ya soka kuwania taji la mataifa bingwa barani Afrika.
Morocco yakanusha madai kuwa inapanga kujiondoa kuwa mwenyeji wa michuano ya soka kuwania taji la mataifa bingwa barani Afrika. AFP PHOTO / ISSOUF SANOGO
Matangazo ya kibiashara

Homa ya Ebola imesababisha zaidi ya watu elfu nne kupoteza maisha nchini Liberia, Sierra Leone na Guinea.

Msemaji wa serikali ya Morroco Mustapha Khalfi, amesema kuwa serikali haitaki kujiondoa ila inataka tu michuano hiyo kuahirishwa kutoka mwezi Januari hadi mwezi Aprili kutokana na hofu ya Ebola.

Shirikisho la soka barani Afrika limesema michuano hiyo haiwezi kuahirishwa kama ilivyopangwa kufanyika kati ya Januari tarehe 17 hadi tarehe 8 mwezi Februari, na tayari imeliandikia barua shirikisho la soka nchini Ghana na Afrika Kusini kutaka kufahamu ikiwa mojawapo ya nchi hizo zinaweza kuwa wenyeji ikiwa Morroco watajiondoa.

Rais wa CAF Issah Hayatou atasafiriki kwenda Morroco mwezi ujao kukutana na viongozi nchini humo kuzungumzia michuano hiyo na tishio la Ebola.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.