Pata taarifa kuu
MICHEZO-RIADHA

Pistorius apoteza umaarufu kufuatia hukumu dhidi yake

Baada ya heshima na utukufu kutokana na kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali, Oscar Pistorius, mwenye umri wa miaka 27, kwa sasa anaoneka kuwa amepoteza umaarufu kutokana na hukumu dhidi yake iliyotolewa leo Jumanne Oktoba 21.

Oscar Pistorius aisabahi familia yake kabla ya kupelekwa jela, Oktoba 21 mwaka 2014.
Oscar Pistorius aisabahi familia yake kabla ya kupelekwa jela, Oktoba 21 mwaka 2014. REUTERS/Herman Verwey/Pool
Matangazo ya kibiashara

Balozi huyo wa Arfika Kusini katika mashindano ya riadha amehukumiwa leo Jumanne mjini Pretoria kifungo cha miaka 5 jela baada ya kupatiakana na hatia ya kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp kwa kumpiga risase bila kukusudia usiku wa siku ya wapendanao mwaka 2013.

Mwanariadha huyo tangu sasa hataonekana katika mashindano mbalimbali ya riadha.
Awali upande wa mashtaka ulimuombea Pistorius adhabu ya kifungo cha miaka 10 jela, lakini upande wa utetezi ulisema haukubaliane na adhabu hio kutokana na ukosefu wa ushahidi wa kutosha na badala yake uliomba Pistorius apewe kifungo cha nyumbani.

Mwakilishi wa Idara ya Magereza ya Afrika Kusini Joel Maringa alipendekeza kuwa Oscar Pistorius aadhibiwe kwa kupewa kifungo cha nyumbani kwa kipindi cha miaka mitatu pamoja na huduma za jamii kwa kupatikana na hatia ya kumuua mchumbake Reeva Steenkamp.

Pistorius ambaye alikua maarufu duniani kwa sasa maisha yake ni riwaya. Pistorius ni mlemavu wa kwanza aliye shiriki katika michezo ya Olimpiki mwaka 2012 mjni London nchini Uingereza. Wakati huo, Oscar Pistorius alipata sifa kimataifa, kwa kukimbia sambamba na na watu wasiokua na ulemavu katika mashindano yaliyotangzwa zaidi duniani.

Oscar Pistorius alipoteza baadhi ya viuogo vya vyake vya miguu akiwa na umri wamiaka 11
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.