Pata taarifa kuu
Timu ya kikapo-Piston-Mchezo

Klabu ya Piston yawatimua baadhi ya wachezaji wake

Timu ya kikapo ya Pistons imemfuta kwenye orodha ya wachezaji wake Hasheem Thabeet, raia wa Tanzania, ambaye alijiunga na timu hiyo mwanzoni mwa mwezi Septemba.

Pistons ikimenyana na Chicago Bulls katika michuano ya preseason, Oktoba 7 mwaka 2014.
Pistons ikimenyana na Chicago Bulls katika michuano ya preseason, Oktoba 7 mwaka 2014. Rick Osentoski-USA TODAY Sports
Matangazo ya kibiashara

Hasheem Thabeet, alijiunga na Pistons, akitokea katika timu ya Philadelphia iliyokuwa imemchukua kutoka klabu ya Oklahoma City Thunder.

Baada ya kujiunga na Pistons, Hasheem Thabeet, ambaye ni raia wa Tanzania alionekana uwanjani mara mbili tu, ambapo, mchezo wake wa kwanza katika michuano ya pre season alicheza dakika tano tu.

Katika mwezi huu wa Oktoba, Hasheem Thabeet amecheza pia dakika tano dhidi ya klabu ya Washington Wizard, ambapo alishindwa kufunga baada ya kupata nafasi nzuri.

Timu ya Pistons imewatimua wachezaji wengine ambao ni Brian Cook, Lorenzo Brown na Josh Bostic kutokana na makosa mbalimbali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.