Pata taarifa kuu
AFRIKA-SOKA-MICHEZO

AFCON 2014: Senegal yajikatia tiketi

Timu ya taifa ya soka ya Senegal, ni miongoni mwa mataifa sita ambayo mwishoni mwa juma lililopita imefuzu katika fainali ya michuano ya soka kuwania taji la Afrika mwaka ujao nchini Equitorial Guinea.

Timu ya taifa ya Senegal imefuzu katika fainali ya michuano ya soka kuwania taji la Afrika mwaka ujao nchini Equitorial Guinea.
Timu ya taifa ya Senegal imefuzu katika fainali ya michuano ya soka kuwania taji la Afrika mwaka ujao nchini Equitorial Guinea. Mamadou Toure Behan / AFP
Matangazo ya kibiashara

Senegal walijahakikishia nafasi hiyo baada ya kuwashinda mabingwa wa zamani Misri bao 1 kwa 0 jijini Cairo na ni wa pili kwa alama 10.

Mataifa mengine ambayo pia yalifuzu Jumamosi iliyopita ni pamoja na Burkina Faso, Cameroon, Gabon, Afrika Kusini na Zambia.

Kabla ya michuano ya mwishoni mwa Juma lililopita, Algeria na Cape Verde walikuwa wamefuzu.

Michuano ya mwisho itachezwa siku ya Jumatano juma hili ambalo mataifa mengine saba yatafuzu.

Matumaoni ya mashabiki wa Afrika Mashariki ni kwa Uganda ambayo mwishoni mwa juma lililopita iliifunga Ghana bao 1 kwa 0 kujiongezea matumani.

Uganda ina alama saba sawa na Guinea. Mataifa haya mawili yatakuwa mjini Casablanca nchini Morroco na atakayeshinda kati yao atafuzu lakini, Uganda wao wanahitaji sare tu ili kufika Equitorial Guinea.

Mara ya mwisho kwa Uganda kucheza katika michuano hii ilikuwa mwaka 1978.

Na Matumaini ya Jamhuri ya Congo kufuzu yalidiidimia baada ya kufungwa na Cameroon bao 1 kwa 0 jijini Yaoude na siku ya Jumatano watacheza na Cote d'Ivoire jijini Abidjan, inabidi washinde kwa mabado mengi ili kuwa na matumaini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.