Pata taarifa kuu
FIFA-Soka-AFCON-michezo

Timu 16 zajiandaa kujielekeza Equatorial Guinea

Raia wa Afrika Mashariki wamekata tamaa, nchi zao kutoshiriki michuano ya kombe la mataifa ya Afrika itakayochezwa Equatorial Guinea, baada ya Uganda kuaga mashindano hayo kwa kufungwa mabao mawili kwa nunge jana Jumatano jioni Novemba  19.

Mchezaji wa Cote d'Ivoire, Serge Aurier (kushoto) akipongezwa na mchezaji wa Cameroon.
Mchezaji wa Cote d'Ivoire, Serge Aurier (kushoto) akipongezwa na mchezaji wa Cameroon. AFP PHOTO / ISSOUF SANOGO
Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo mabingwa watetezi Nigeria imetupwa nje baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 na Afrika Kusini. Congo Brazaville imejiunga na mataifa mengine yaliyofuzu ambayo yatashiriki michuano ya kombe la mataifa ya Afika itakayo anza Januari 17 nchini Equatoria Guinea, baada ya Mashetani wekundu kufanya vizuri.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imekata tiketi ya kushiriki michuano ya kombe la mataifa ya Afrika baada ya kumaliza michuano hiyo ikiwa na alama 9, huku ikichukua nafasi ya tatu. Cameroon na Cote d’Ivoire zimetoka sare ya kutofungana.

Nchi kumi na sita ndio zimejulikana kuwa zitashiriki michuano hiyo ya kombe la mataifa ya Afrika itakayochezwa tangu Januari 17 hadi februari 8 mwaka 2014 nchini Equatorial Guinea.

Itafahamika kwamba Equatorial Guinea ambayo ni mwenyeji wa michuano hiyo, baada ya Morocco kujiondoa, itashiriki michuano hiyo. Misri imelambishwa mabao mawili kwa nunge na Tunisia.

Congo, Côte d’Ivoire, Guinea, Mali, Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo zimefuzu na kwa sasa zimejiunga na Algeria, Burkina Faso, Cameroon, Gabon, Senegal, Tunisia, Afrika Kusini, Cape Verde, Ghana, Zambia na Equatorial Guinea, ni nchi 16 ambazo zitashiriki michuano ya kombe la mataifa ya Afrika. Nchi zaidi ya kumi miongoni mwa nchi hizo 16 zinazungumza Kifaransa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.