Pata taarifa kuu
LIGI YA MABINGWA / ULAYA

Ligi ya mabingwa: Manchester City yaibwagiza Bayern

Manchester City imefaulu kuishinda Bayern kwa mabao 3-2, baada ya Agüero kuweka wavuni bao la ushindi. Yaya Touré hakucheza mchuano wa Jana Jumatano Novemba 25. Hata hivyo Manchester City imefanya vizuri ikiwa nyumbani na kufuzu katika mzunguko wa nane wa ligi ya mabingwa.

Sergio Agüero, mchezaji wa Manchester City, aliye funga mabao 3 dhidi ya Bayern Munich ya Ujerumani.
Sergio Agüero, mchezaji wa Manchester City, aliye funga mabao 3 dhidi ya Bayern Munich ya Ujerumani. REUTERS/Phil Noble
Matangazo ya kibiashara

Machester City ilianza vibaya katika mchuano huo, kufuatia kukosekana uwanjani kwa Yaya Touré, ambaye aliondolewa uwanjani katika mechi iliyotangulia baada ya kupewa kadi nyekundu.

Katika dakika ya 20 ya mchezo, Medhi Benatia, beki wa kati wa Bayern, alimfanyia madhambi mchezaji wa manchester City, Agüero, na mwamuzi akaamua itengwe penalti, baada ya Medhi Benatia, kutoka Morocco kupewa kadi nyekundu. Penalti hiyo iliingizwa wavuni na Agüero, na kupelekea Manchester kuongoza kwa bao 1-0.

Licha ya kuwa idadi ya wachezaji ilikua imepungua, Bayen ilikuja juu na kusawazisha katika dakika ya 40. Bao hilo lilwekwa kimyani na Xabi Alonso. Baada ya dakika 5, Bayern iliingiza bao la pili, na kuongoza ikiwa na mabao 2-1.

Hadi mwisho wa kipindi cha kwanza cha mchezo, Bayern ilikua ikiongoza kwa mabao 2-1. Lakini hali ya mchezo ilibadilika, wakati ambapo Bayern ilikosa mabao mengi, huku  Xabi Alonso, akipoteza mpira, na kuchukuliwa na Agüero, ambaye alifaulu kuingiza bao la pili na kupelekea klabu yake ya Manchester City kuwa sare ya mabao 2-2 na Bayern. Bao hilo la kusawazisha liliingizwa wavuni katika dakika ya 85.

Agüero alifaulu katika dakika ya 90 kuingiza bao la ushindi, na kupelekea Manchester City kuishinda bayern mabao 3-2.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.