Pata taarifa kuu
AFRIKA-CAF-SOKA-AFCON 2015-MICHEZO

Timu ya taifa ya Algeria yatangaza kikosi chake

Timu ya taifa ya soka ya Algeria imekuwa ya kwanza kutangaza kikosi chake cha wachezaji 23 kitakachoshiriki katika mechi za mataifa bingwa barani Afrika mwaka ujao nchini Equitorial Guinea.

Ryad Boudebouz ni mmoja kati ya wachezaji 7 wa ziada wa kikosi cha timu ya taifa ya Algeria kitakacho shiriki michuano ya Kombe la mataifa barani Afrika mwaka 2015, nchini Equatorial Guinea.
Ryad Boudebouz ni mmoja kati ya wachezaji 7 wa ziada wa kikosi cha timu ya taifa ya Algeria kitakacho shiriki michuano ya Kombe la mataifa barani Afrika mwaka 2015, nchini Equatorial Guinea. AFP PHOTO / PASCAL POCHARD-CASABIANCA
Matangazo ya kibiashara

Kocha Christian Gourcuff amemtaja kiungo wa kati wa klabu ya Newcastle United ya Uingereza, Mehdi Abeid.

Abeid mweye umri wa miaka 22 na ambaye hajawahi kuichezea timu ya taifa, ni miongoni mwa wachezaji watano wapya waliopata nafasi katika kikosi hicho.
Algeria ipo katika kundi la C pamoja na Ghana, Senegal na Afrika Kusini.

Hivi ndivyo ratiba itakavyokuwa katika kundi hili wakati michuano hiyo itakapoanza tarehe 17 mwezi Januari na kumalizika tarehe 8 mwezi Februari.

Mechi za Algeria katika Michuano ya mataifa bingwa barani Afrika 2015 :

19 Januari : Algeria v South Africa itachezwa Mongomo
23 Januari : Algeria v Ghana  itachezwa Mongomo
27 Januari : Algeria v Senegal  itachezwa Malabo

Wachezaji wengine ambao wameitwa kwa mara ya kwanza katika kikosi hiki ni pamoja na, Ishak Belfodil, Foued Kadir, goli kipa Doukha Izzeddine na Mehdi Zeffane.

Kikosi kamili ni:

Makipa : Rais Mbolhi (Philadelphia Union, USA)), Doukha Izzeddine (JS Kabylie) Mohamed Lamine Zemmamouche (USM Alger).

Mabeki : Essaid Belkalem (Trabzonspor, Turkey), Madjid Bougherra (Fujaira, UAE), Faouzi Ghoualm (Napoli, Italy), Rafik Halliche (SC Qatar, Qatar), Aissa Mandi (Stade Reims, Ufaransa), Carl Medjani (Trabzonspor, Turkey), Djamel Mesbah (Sampdoria, Italy), Mehdi Zeffane (Lyon, Ufaransa)

Viungo wa Kati : Nabil Bentaleb (Tottenham, England), Yacine Brahimi (Porto, Ureno), Medhi Lacen (Getafe, Uhispania), Saphir Taider (Sassuolo, Italia), Mehdi Abeid (Newcastle United, Uingereza), Foued Kadir (Real Betis, Uhispania)

Washambuliaji : Abdelmoumene Djabou (Club Africain, Tunisia), Sofiane Feghouli (Valencia, Uhispania), Riyad Mahrez (Leicester City, Uingereza), Islam Slimani (Sporting Lisbon, Ureno), Hilal Soudani (Dinamo Zagreb, Croatia), Ishak Belfodil (Parma, Italia)

Wachezaji wa ziada : Liassine Cadamuro (Osasuna, Uhispania), Adlene Guedioura Adlane (Watford, Uingereza), Mehdi Mostefa (Lorient, Ufaransa), Walid Mesloub (Lorient, Ufaransa), Ryad Boudebouz (SC Bastia, Ufaransa), Ahmed Kashi (Metz, Ufaransa), Baghdad Bounedjah (Etoile du Sahel, Tunisia).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.