Pata taarifa kuu
TANZANIA-CAF-SOKA-

CAF : Tanzania mwenyeji wa michuano ya vijana chipukizi

Shirikisho la soka barani Afrika CAF limeiteua Tanzania kuwa mwenyeji wa michuano ya vijana chipukizi wasiozidi miaka 17 mwaka 2019.

Mwenyekiti wa Shirikisho la Soka barani Afrika CAF, Issa Hayatou.
Mwenyekiti wa Shirikisho la Soka barani Afrika CAF, Issa Hayatou. AFP PHOTO / STEPHANE DE SAKUTIN
Matangazo ya kibiashara

Mwenyekiti wa Shirikisho la soka nchini Tanzania Jamal Malinzi amesema uongozi wa soka umefurahishwa na uamuzi wa CAF.

“ Kuwa wenyeji wa michuano hii ya vijana barani Afrika ni ishara kuwa ipo siku tutaanda michuano ya mataifa bingwa barani Afrika AFCON siku zijazo”, amesema.

Jamal ameongeza kuwa hii ni changamoto kwa Shirikisho hilo kuanza kuandaa kikosi kitakachoshiriki katika michuano hiyo lakini kwanza ni kuunda kikosi cha wachezaji wasiozidi miaka 13 watakaoshiriki katika michuano ya Afrika mwaka 2015.

Habari hii kutoka CAF imepokelewa kwa furaha kubwa na wadau wa soka nchini humo ambao wanasema Tanzania sasa ina nafasi ya kuonesha vipaji vyake na uwezo wa kuwa wenyeji wa michuani hii mikubwa barani Afrika.

Tanzania inajivunia uwanja wa kisasa wa Taifa jijini Dar es salaam, ule Chamazi nje kidogo jiji la Dar es salaam na CCM Kirumba mjini Mwanza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.