Pata taarifa kuu
WIMBLEDON-TENESI

Djokovic, Serena, Sharapova wafungua pazia la michuano ya tenesi ya Wimbledon nchini Uingereza

Wachezaji, Novak Djokovic, Serena Williams na Maria Sharapova hii leo wanatarajiwa kuanza kutupa karata zao za kwanza kwenye michuano ya tenesi ya Wimbledon, huku mchezaji Lleyton Hewitt akitarajia kuaga mashabiki katika michuano hii ya 17 ya Wimbledon.

Mserbia, Novak Djokovic mchezaji nambari moja kwa ubora wa mchezo wa Tenesi duniani
Mserbia, Novak Djokovic mchezaji nambari moja kwa ubora wa mchezo wa Tenesi duniani Reuters/Suzanne Plunkett
Matangazo ya kibiashara

Mchezaji nambari moja wa mchezo huo, na bingwa mtetezi wa michuano ya Wimbledon, Novak Djokovic atacheza mechi yake ya kwanza toka pale mchezaji Stan Wawrinka alipomfunga na kuzima ndoto zake kwenye michuano French Open majuma matatu yaliyopita.

Mserbia, Djokovic ambaye ni bingwa wa michuano ya Wimbledon mwaka 2011, hajawahi kushindwa kwenye mchuano wake wa kwanza wa michuano hii, lakini anakabiliana na mpinzani wake anayepewa nafasi Philipp Kohlscheiber ambaye mwaka 2012 alifika hatua ya robo fainali na anashikilia nafasi ya 33 kwa ubora wa mchezo huo.

Djokovic anashikilia rekodi nzuri dhidi ya mpinzani wake raia wa Ujerumani ambaye kwenye michuano iliyopita alimfungwa kwa seti moja kwa matokeo ya 6-1.

Kwa upande wa wanawake, mchezaji nambari moja kwa mchezo huo, Serena Williams bingw amara tano wa michuano ya Wimbledon, ataanza mchezo wake wa kwanza na mrusi, Magarita Gasparyan ambaye yuko nafasi ya 113 kwa mchezo huo upande wa wanawake.

Mrusi, Magarita ameshashiriki mara moja tu kwenye michuano mikubwa kama hii, ambapo mara ya kwanza alipoteza mchezo wake wa kwanza kwenye michuano ya French Open ya mwaka huu.

Williams ambaye ameshinda taji la Australian na French Open katika kipindi cha miezi sita iliyopita, na sasa anatarajiwa kurejea tena kwenye uga wa wachezaji mahiri wa michuano ya Wimbledon na huenda akawa mwanamke wa kwanza baada ya Seffi Graf mwaka 1988 kushinda taji lake la nne katika kipindi cha mwaka mmoja.

Serena mwenye umri wa miaka 33, ameshinda taji la US Openi la mwaka 2014 kwa kishindo na anapewa nafasi kubwa ya kushinda taji lake la sita la michuano hii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.