Pata taarifa kuu
FIFA-USWIS-MAREKANI

Uswisi: " Tumepokea maombi toka Serikali ya Marekani "

Serikali ya Uswisi hii leo imethibitisha kupokea maombi rasmi kutoka kwa Serikali ya Marekani ikiomba kupelekwa nchini humo kwa maofisa 7 wa shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA, waliokamatwa May 27 mwaka huu mjini Zurich kwa tuhuma za rushwa.

Makao makuu ya FIFA yaliyoko mjini Zurich, Uswis
Makao makuu ya FIFA yaliyoko mjini Zurich, Uswis REUTERS/Ruben Sprich/Files
Matangazo ya kibiashara

Katika tangazo lililotolewa na ofisi ya mwendesha mashtaka wa Uswisi, imesema kuwa ubalozi wa Marekani mjini Bern umetuma maombi rasmi kwenye ofisi yake ukiomba kupelekwa kwa watuhumiwa hao 7 kulingana na muda uliopo na kwa makubalino ya ushirikiano wa kubadilishana watuhumiwa kati ya nchi hizo mbili.

Serikali ya Marekani inayo siku chache za kuwasilisha maombi rasmi katika barua kuomba kupelekwa kwa watuhumiwa hao, ambapo kwa mujibu wa makubaliano yao, Marekani inapaswa kuwa imewasilisha maombi hayo mpaka kufikia July 3 mwaka huu au kuomba kusogeza mbele ombi lao.

Maofisa hao 7 wa FIFA na washirika wake, walikamatwa May 27 mwaka huu mjini Zurich saa chache kabla ya kuanza kwa mkutano mkuu wa FIFA ambapo watu wote hao saba wamekuwa kizuizini kwa maombi ya Marekani.

Hati ya mashtaka ya Marekani imejikita katika hati ya kukamatwa kwa watu hao iliyotolewa May 20 na mwendesha mashtaka wa New York, ambaye kwenye hati yake alidai watu hao wanatuhumiwa kwa makosa ya kukubali na kupokea rushwa ya zaidi ya dola milioni 100.

Kwa mujibu wa hati hiyo, rushwa hii ilitolewa kwa wawakilishi wa masuala ya soka, vyombo vya habari vya michezo, watu wa matangazo na taasisi nyingine za ahabari ili kupewa haki ya kurusha michuano ya kombe la dunia, Amerika Kusini.

Hatua hii imekuja baada ya Serikali ya Marekani kuanzisha uchunguzi rasmi dhidi ya maofisa kadhaa wa FIFA akiwemo rais wa sasa Sepp Blatter ambaye ametangaza kuwa atakaa kando na kuitisha mkutano mwingine mkuu wa dharura kuchagua viongozi wapya.

Miongoni mwa kashfa nyingine za rushwa zinazochunguzwa na maofisa wa Marekani na wale wa Uswisi ni pamoja na upewaji wa zabuni kwa nchi ya Afrika Kusini ilipoandaa fainali za mwaka 2010, lakini utolewaji wa zabuni kwa nchi za Urusi na Qatar kuandaa fainali za kombe la dunia za mwaka 2018 na 2022.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.