Pata taarifa kuu
CECAFA-SOKA

Michuano ya CECAFA yatazamiwa kuchezwa Dar es Salaam

Makala ya 41 kuwania taji la klabu bingwa katika nchi za Afrika Mashariki na Kati CECAFA maarufu kwa jina la Kagame Cup, yanaanza kutimua vumbi kuanzia tarehe 18 hadi tarehe 2 mwezi Agosti jijini Dar es salaam nchini Tanzania.

Uwanja wa taifa wa soka Dar Es Salaam, Tanzania.
Uwanja wa taifa wa soka Dar Es Salaam, Tanzania. YOUTUBE
Matangazo ya kibiashara

RFI inathathmini vlabu 13 vitakavyoshiriki katika kindumbwendubwe hiki kinacholenga kuleta ushindani wa soka eneo la Afrika Mashariki na Kati na kuinua kiwango cha mchezo.

Mabingwa mara 6 Simba FC kutoka Tanzania na mabingwa watetezi Al Mereikh ya Sudan hawatashiriki katika michuano ya mwaka huu, baada ya Simba kutofuzu na Al Mereikh kujiondoa.

Droo ya michuano hii ilipofanyika jijini Dar es salaam, hakuna aliyefahamu kuwa mchuano wa ufunguzi ungekuwa kama wa fainali.

Mabingwa wa soka nchini Tanzana Yanga, wameratibiwa kufungua michuano hii dhidi ya Gor Mahia ya Kenya baada ya kujumuishwa katika kundi moja.

Licha ya soka la uwanjani pia tunatarajia kuona ushindani wa mashabiki wa Yanga na Gor Mahia, ambao wamekuwa wakionesha mapenzi makubwa kwa timu zao.

Mashabiki wa Yanga wanajivunia kuwa nyumbani na tunatarajia kuwaona kwa maelfu wakifurahika katika uwanja wa taifa huku wale wa Gor Mahia wakiwasili kwa mamia kutumia usafiri wa mabasi kutoka jijini Nairobi.

Droo ilivyopangwa

Kundi A-Gor Mahia(Kenya) ,Yanga (Tanzania), Al Khartoum SC(Sudan), KMKM (Zanzibar) na Telecom(Djibouti)

Hili linaonekana kuwa gumu sana kutokana na kuwepo kwa miamba wa soka wa Tanzania Yanga na Gor Mahia kutoka Kenya, lakini katika kundi kama hili vlabu ambavyo huwa havipewi nafasi huwa vinachomoza na kufanya vizuri.

Al Khartoum inayofunzwa na kocha wa zamani wa Ghana Kwesi Appiah sio ya kudharauliwa pamoja na mabingwa wa soka Zanzibar KMKM ambao wanafahamika kwa kasi na kucheza pasi fupifupi.

1-Historia ya Young Africans (Yanga)-Tanzania

Inafahamika kwa jina la utani kuwa Jangwani Boys, kutokana na makao makuu kuwa katika eneo la Jagwani jijini Dar es salaam.

Iliundwa mwaka 1935.

Watani wao wa jadi katika soka la Tanzania ni Simba FC alimaarufu vijana wa Msimbazi.

Imeshinda mataji ya CECAFA mara 5. Mara ya mwisho kunyakua taji ilikuwa ni mwaka 2011 na 2012 walipozifunga Simba na Azam FC zote za Tanzania.

Kocha wa sasa ni Hans De Pluijm kutoka Uholanzi.
Wachezaji wa kutegemewa Haruna Niyonzima na Andrey Coutinho.


2- Gor Mahia (Kenya)

Makao makuu ni jijini Nairobi.

Ilishinda taji la Mandela barani Afrika mwaka 1987 ambalo siku hizi linaitawa Shirikisho.

Wameshinda mataji 3 ya CECAFA.

Kocha Mkuu ni Frank Nuttal kutoka Uingereza.

Wachezaji wa kutegemewa ni pamoja na Michael Olunga, Paul Were na Meddie Kagere wote ni washambuliaji.

3-Al Khartoum SC(Sudan)

Ilichukua nafasi ya mabingwa watetezi Al Mereikh waliojiondoa.

Zamani walikuwa wanafahamika kwa jina la Al Khartoum 3 na klabu hii inajivunia wachezaji wa kulipwa akiwemo Teddy Akumu zamani aliichezea Gor Mahia ya Kenya na Leonard Njousso wa Cameroon.

Kocha wa klabu hii ni Mghana, James Kwesi Appiah zamani akiifunza timu ya taifa ya Ghana.

Walimaliza katika nafasi ya 4 katika ligi kuu ya soka nchini Sudan.

4-AS Ali Sahieh Djibouti Telecom (Djibouti)

Imeshinda mataji 4 katika ligi ya soka nyumbani.

Mwaka 2014 wakati wa michuano ya CECAFA iliishinda KCCA ya Uganda mabao 2 kwa 1.

Wachezaji wa kuangaliwa ni pamoja na Mohammed Mustapha na Aboubala Djama.

5-Kikosi Maalum Cha Kuzuia Magendo (KMKM)-Zanzibar

Mabingwa wa soka nchini Tanzania 1984 kabla ya Zanzibar kuanza ligi yake.

Wameshinda ligi ya Zanzibar mara 4.

Uwanja wao wa nyumbani ni Unguja Park.

Mwaka 2014 walikuwa na wakati mgumu katika michuano ya CECAFA walifungwa na Rayon Sport ya Rwanda bao 1 kwa 0 , huku ndugu zao Azam mabao 4 kwa 0.

Wachezaji wa kuangaliwa Mudrik Abdul na Ali Shibol Ali.

Kundi B-APR (Rwanda), Al Ahly Shendy (Sudan), LLB Academic (Burundi) and Heegan FC (Somalia)

Kundi hili pia linaangaziwa kuwa miongoni mwa makundi ya kifo kutokana na uwepo wa APR iliyofika fainali mwaka jana pamoja na Lydia Ludic Academic ya Burundi imekuwa ikifanya vizuri katika siku za hivi karibuni pia barani Afrika.

Al Ahly Shendy ya Sudan ambao imekuwa ikishiriki katika michuano ya bara Afrika pia inatarajiwa kuleta ushindani mkali.

1- APR (Rwanda)

Klabu ya kijeshi, Armée Patriotique Rwandaise.

Ilianzishwa mwaka 1993.

Uwanja wa nyumbani ni Amahoro jijini Kigali

Mabingwa wa CECAFA mara 3.

Mwaka 2014 walifika fainali na kufungwa na Al Mereikh ya Sudan.

Walipoteza pia katika hatua ya fainali mwaka 1996 na 2000.

2- Al Ahly Shendy (Sudan)

Makao ya klabu hii ni mjini Shendy nchini Sudan

Ilianzishwa mwaka 1943.

Mwaka 2012 ilishiriki michuano ya Shirikisho barani Afrika na kufika hatua ya makundi.

3-Lydia Ludic Burundi Academic (LLB Academic FC)

Mabingwa wa soka nchini Burundi mwaka 2014.

Uwanja wa nyumbani ni Prince Louis Rwagasore jijini Bujumbura.

Mwaka 2012 ilifika hatua ya nane bora kuwania taji la Shirikisho barani Afrika baada ya kushinda DC Motema Pembe mabao 2 kwa 1.

Wachezaji wa kutegemewa Christophe Nduwarugira, Shasiri Nahimana na Issa Hakizimana.

4-Heegan FC (Somalia)

Ilianzishwa mwaka 1960.

Mabingwa wa ligi kuu nchini Somalia mara 2 mara ya mwisho mwaka 2014/15
Uwanja wa nyumbani ni Benadir.

Wachezaji wa kutegemewa ni pamoja na Jibril Hassan Mohammed na Sidi Mohammed Oman.

Group C– Azam FC (Tanzania), Al Malakia (SSDN), Adama City (Ethiopia), KCCA (Uganda)

Kundi hili pia ni gumu katika michuano ya mwaka huu.

Mchuano wa Azam FC na KCCA wa Uganda utakuwa wa kuvutia.

Azam pia watakuwa nyumbani na kupata uungwaji wa mashabiki wa nyumbani.

Adama City na Al Malakia vina uzoefu mkubwa katika michuano hii.

KCCA wana uzoefu katika michuano hii.

5-Azam FC (Tanzania)

Ilianzishwa mwaka 2007.

Klabu hii inajivunia utajiri wa fedha kutokana na mmiliki kuwa mfanyibiashara Abubakar Bakhresa.

Hawajawahi kunyakua ubingwa wa CECAFA.

Waliwahi kufika fainali ya michuano hii mwaka 2013 na kufungwa na ndugu zao Yanga mwaka 2012.

Uwanja wao wa nyumbani ni Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.

Mabingwa mara mbili wa ligi ya Tanzania bara 2013 na 2014.

1-Adama City (Ethiopia)

Ilianzishwa mwaka 1991.

Uwanja wa nyumbani ni Adama
.
Ilichukua nafasi ya St George baada ya kujiondoa.

 

2-Al Malakia (South Sudan)

Ilianzishwa mwaka 1945.

Ilikuwa inashiriki ligi ya Sudan kabla yanchi yao kujitenga 2011.

Mabingwa wa soka nchini Sudan Kusini mwaka 2013/2014.

Haijawahi kushiriki katika michuano ya CECAFA.

Klabu ya kwanza kucheza katika michuano ya kutoka Sudan Kusini CECAFA ni Al Nasr.

3-KCCA (Uganda)

Mabingwa soka nchini Uganda 2013/2014

Walishinda taji la CECAFA mwaka 1978.

Makao yao makuu ni jijini Kampala, katika uwanja wa Lugogo.

Wemenyakua ligi mara 10 nyumbani.

Kocha ni Sam Ssimbwa.

Wachezaji wa kutegemewa Francis Olaki na Ronnie Kisehka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.