Pata taarifa kuu
CECAFA-KENYA-SUDAN-GOR MAHIA-AL KHARTOUM-SOKA

Gor Mahia na Al Khartoum zafuzu katika hatua ya nusu fainali

Gor Mahia ya Kenya na Al Khartoum ya Sudan zimefuzu katika hatua ya nusu fainali kuwania taji la klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati CECAFA baada ya ushindi katika hatua ya robo fainali siku ya Jumanne katika uwanja wa taifa wa Dar es Salaam nchini Tanzania.

Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Tanzania, ambako zinachezwa mechi ya kuwania taji la klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati CECAFA.
Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Tanzania, ambako zinachezwa mechi ya kuwania taji la klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati CECAFA. Emmanuel Makundi, RFI Journalist
Matangazo ya kibiashara

Al Khartoum inayofunzwa na kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Ghana Kwesi Apiah, ilipata ushindi mkubwa wa mabao 4 kwa 0 katika mchuano huo.

Bao la ufunguzi la Al Khartoum lilitiwa kimyani na mchezaji Atif Khalid katika dakika 10 ya mchuano huo, huku Amin Ibrahim akifunga bao la pili katika dakika ya 20 na la tatu katika dakika ya 40, huku Osman Salaheldin akimaliza kazi kwa kuipa ushindi klabu yake bao la nne.

Kocha Appiah amesema kuwa mabao ya mapema yaliisaidia timu yake kuendelea kujiimarisha katika mchuano huo.

Katika mchuano mwingine, mabingwa wa Kenya Gor Mahia walipata ushindi wa mabao 2 kwa 1 dhidhi ya Malakia ya Sudan Kusini.

Gor Mahia ilipata bao lake la ufunguzi kupitia Godfrey Walusimbi katika dakika za mapema za mchuano huo ulionekana mgumu kwa vijana kutoka Kenya katika kipindi cha pili.

Mabingwa hao wa Kenya sasa watacheza na Al Khartoum katika hatua ya nusu fainali.

Leo Jumatano, Al Shandy washindi wa pili wa kundi B watachuana na KCCA ya Uganda waliomaliza wa pili katika kundi C kwa alama 6.

Mchuano unaosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka nchini Tanzania ni kati ya Azam na Yanga, mchuano ambao kwa mashabiki wa timu hizi mbili umekuja mapema na ni kama fainali ya mwaka 2013.

Fainali ya michuano hii ya CECAFA itachezwa siku ya Jumapili mwishoni mwa juma hili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.