Pata taarifa kuu
AFRIKA-CAF-SOKA

Nchi zitakazoshiriki michuano ya soka kuwania ubingwa wa Afrika

Mataifa saba ya Afrika yatakayoshiriki katika michuano ya soka kuwania ubingwa wa Afrika kwa wachezaji wasiozidi miaka 23 itakayofanyika kati ya tarehe 28 mwezi Novemba hadi tarehe 12 mwezi Desemba nchini Senegal yameshafahamika rasmi.

Mchuano wa fainali wa Ligi ya Mabingwa CAF 2010 kati ya Esperance Tunis na Tout Puissant Mazembe.
Mchuano wa fainali wa Ligi ya Mabingwa CAF 2010 kati ya Esperance Tunis na Tout Puissant Mazembe. AFP PHOTO / FETHI BELAID
Matangazo ya kibiashara

Mataifa hayo ni pamoja na wenyeji Senegal, Algeria, Misri, Zambia, Tunisia, Afrika Kusini, Nigeria na Mali.

Zambia, Tunisia na Mali zimefuzu katika michuano hii kwa mara ya kwanza.
Michuano ya mwisho ya kufuzu ilichezwa mwishoni mwa juma lililopita na washindi kupatikana.

Nigeria ilifuzu baada ya kuifunga Congo Brazaville mabao 2 kwa 1.

Algeria iliishinda Sierra Leone mabao 2 kwa 0, huku Mali ikiilaza Gabon mabao kwa 0.
Vijana wa Misri, waliwachabanga Uganda mabao 6 kwa 1, baada ya kushindwa mabao 4 kwa 0 jijini Cairo na nyumbani kulemewa kwa mabao 2 kwa 1.

Afrika Kusini nayo iliishinda Zimbabwe kwa jumla ya mabao 4 kwa 1, huku Tunisia wakiwalemea Morocco mabao 2 kwa 1.

Zambia baada ya kutoka sare ya kutofungana na Cote d'Ivoire nyumbani na ugenini ilifuzu baada ya kupata ushindi wa penalti 4 kwa 3.

Michuano hiyo pia itatumiwa kutafuta timu tatu za kwanza kufuzu katika michezo ya msimu joto ya Olimpiki itakayofanyika nchini Brazil mwaka ujao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.