Pata taarifa kuu
CHAN-RWANDA

Nusu fainali ya kwanza ya michuano ya CHAN kupigwa hii leo, DRC inakibarua dhidi ya Guinea

Mechi za nusu ya kwanza ya michuano ya kombe la mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za nyumbani, zinatarajiwa kupigwa hii leo jijini KIgali, Rwanda.

Timu ya taifa ya Côte d'Ivoire katika michuano ya CHAN 2016.
Timu ya taifa ya Côte d'Ivoire katika michuano ya CHAN 2016. Courtesy of cafonline
Matangazo ya kibiashara

Nusu fainali ya kwanza inatarajiwa kupingwa hii leo kwenye dimba la Amahoro mjini Kigali, ambapo timu ya taifa ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, DRC, itakuwa na kibarua dhidi ya timu ya taifa ya Guinea.

Timu ya taifa ya Guinea, maarufu kama The Syli Nationale, inashiriki kwa mara ya kwanza kwenye michuano ya mwaka huu, huku ikifika kwenye hatua hii baada ya kuwafunga Zambia kwenye hatua ya robo fainali kwa juma ya penalty 5-4.

Baada ya kuokoa penalty ya Zambia, mlinda mlango wa Guinea, Abdul Aziz Keita aliifungia timu yake penalty ya ushindi na kuipeleka timu yake ya taifa katika hatua ya nusu fainali.

Timu ya taifa ya DRC yenyewe itaingia uwanjani ikijivunia wachezaji kutoka timu mbili kubwa nchini DRC, ambazo ni TP Mazembe na AS Vita Club, ambapo haitakuwa na mshambuliaji wake mahiri, Heritier Luvumbu.

Mechi nyingine ya nusu fainali ya pili inatarajiwa kupigwa hapo kesho katika dimba la Stade de Kigali ambapo timu ya taifa ya Ivory Coast itakuwa na kibarua dhidi ya timu ya taifa ya Mali.

Ivory Coast walitinga kwenye hatua hii baada ya kuwafunga Cameron kwa mabao 3-0, huku mali wao wakitinga kwenye hatua hii baada ya kuifunga timu ya taifa ya Tunisia kwa mabao 2-1.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.