Pata taarifa kuu
NGUMI

Bingwa wa dunia wa uzito wa juu, Tyson Fury asema huenda akastaafu kucheza ngumi, adaiwa kutaka kumkwepa Klitschiko

Bingwa dunia wa uzito wa juu, Tyson Fury amesema kuwa bado hajaamua iwapo atapigana tena na mpinzani wake, Wladimir Klitschko na kwamba bada yake huenda akaachana na mchezo huo.

Tyson Fury akiwa na mikanda yake ya ubingwa baada ya kumpiga mpinzani wake, Wladimir Klitschko
Tyson Fury akiwa na mikanda yake ya ubingwa baada ya kumpiga mpinzani wake, Wladimir Klitschko Reuters
Matangazo ya kibiashara

Fury alimpiga Klitschko na kutwaa mataji ya WBA, IBF na WBO mwezi November mwaka jana na hivi karibuni huenda akarejea tena ulingoni kutetea taji lake kwa mara nyingine mwezi May au June mwaka huu.

Akihojiwa na kituo kimoja cha redio nchini Uingereza, Fury anasema kuwa anapata shida sana kuamua iwapo apigane tena au la, na kwamba huenda asipigane na kustaafu huku akiwa hajapoteza pambano lolote.

Tyson Fury
Tyson Fury Reuters / Lee Smith Livepic

Fury ameongeza kuwa licha ya kuwa mchezo wa masumbwi unaangalia hela zaidi, lakini kwake hivi sasa ni tofauti na anataka kufanya mchezo huu kwake usiwe ni kuangalia kiasi cha fedha anachopokea.

Amesema ameshatimiza ndoto yake kwa kumpiga Klitschiko, na hivyo ni kitu gani kingine kimesalia kwa yeye kukimalisha zaidi ya kustaafu masumbwi.

Fury anasema kuna maisha baada ya mchezo wa ngumi, na kwamba hafahamu kitu gani kitatokea mbele, na hata hivyo hajaamua iwapo atapigana tena au la, huku kwa mara ya kwanza akisema kuwa hajafanya mazoezi toka wakati huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.