Pata taarifa kuu
CHAN-RWANDA

DRC yafuzu hatua ya fainali michuano ya CHAN, leo ni zamu ya Mali na Ivory Coast

Michuano ya kombe la mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za nyumbani maarufu kama CHAN, imeshika kasi nchini Rwanda, ambapo sasa ni hatua ya nusu fainali, huku DRC ikitinga hatua ya fainali baada ya kuwafunga Guinea.

Nahodha wa timu ya taifa ya DRC inayoshiriki michuano ya CHAN nchini Rwanda, Joel Kimwaki akishangilia
Nahodha wa timu ya taifa ya DRC inayoshiriki michuano ya CHAN nchini Rwanda, Joel Kimwaki akishangilia CAF
Matangazo ya kibiashara

Ndoto ya timu ya taifa ya Guinea kufika hatua ya fainali kwenye michuano ya mwaka huu ilifutika siku ya Jumatano ya wiki hii, baada ya kukubali kuondoshwa kwenye hatua ya nusu fainali kwa mikwaju ya penalty 5-4 kutoka kwa timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC.

Mchezaji wa DRC, Meschack Elia ndiye aliyeifungua timu yake penalty ya ushindi na kuipeleka DRC kwenye hatua ya fainali siku ya Jumapili, ambapo itakutana na mshindi wa mechi ya leo kati ya Mali na Ivory Coast.

DRC ilikuwa ya kwanza kupata bao katika muda wa nyongeza kupitia kwa Jonathan Bolingo bao ambalo wakayi dakika zikiyoyoma, mchezaji wa Mali, Ibrahima Sankhon aliifungua bao la kusawazisha timu yake na kufufua matumain ya kufika fainali.

Timu ya taifa ya Côte d'Ivoire katika michuano ya CHAN 2016.
Timu ya taifa ya Côte d'Ivoire katika michuano ya CHAN 2016. Courtesy of cafonline

Timu ya taifa ya Guinea, ikiwa ni mara yake ya kwanza kushiriki mashindano ya mwaka huu toka nchi yao ilipokumbwa na ugonjwa wa Ebola, ilionesha kandanda safi toka kipindi cha kwanza cha mchezo hadi hatua ya muda wa nyongeza.

Mashuti ya Moussa Diawara na Sankoh hayakufua dafu mbele ya mlinda mlango wa DRC, Ley Matampi ambaye aliokoa michomo yao kwa umahiri mkubwa na kuendelea kubeba matumaini ya "Leopards".

Hii leo pia kutakuwa na mechi nyingine na ya mwisho ya nusu fainali ya CHAN, ambapo timu ya taifa ya Mali itakuwa na kibarua dhidi ya timu ya taifa ya Ivory Coast, kwenye mchezo ambao unatajwa kuwa mgumu kutokana na umahiri wa timu zote mbili.

Mali inajivunia viungo wae wakabaji na washambuliaji wenye nguvu na kasi ambao toka hatua ya makundi wameonesha umilikaji mkubwa wa mpira na kuwasumbua mabeki wa timu pinzani.

Ivory Coast nao wanajivunia kuwa na ukuta mgumu usiopitika kirahisi pamoja na washambuliaji wake wenye kazi ambao mara zote wamekuwa mwimba kwa timu pinzani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.