Mjumbe

Kwa zaidi ya miaka kumi RFI imemteua mjumbe. Kuonyesha umuhimu ambao RFI inao kwa ubora wa uhusiano wake na wasikilizaji pamoja na watumiaji wa Tovuti. Mjumbe ni msemaji wa umma kwa waandishi wa habari na wa Uongozi. Yuko pale ya kupokea malalamiko, maswali, pongezi na pia kujibu, kuhalalisha, kuelezea au kuomba radhi kwa dhati na taadhima.
Tangu alipoingia RFI mwaka 1988, Dominique Burg anajua vizuri kampuni, historia yake na waandishi wake wa habari.
Amekuwa msimamizi wa sera na huduma wa Ufaransa, na baadaye Mhariri wa sera.
Tangu mwaka 2005, alikuwa mhariri mtendaji wa Kifaransa. Ana, zaidi ya hayo, kwa muda mrefu uzoefu wa kitaaluma, tajiri kwa kuweza kupitia aina zote za vyombo vya habari: magazeti ya kila siku, gazeti Le Quotidien ya Paris na Le Matin ya Paris, Taasisi kuu ya vyombo vya habari, magazeti ya kila wiki, kama l’Evenement du jeudi, na televisheni, baada ya kushiriki katika kubuni na kuendeleza Runinga ya Bunge.
Raia wa Dauphine, katika Milima, Dominique Burg ni msomi na an shaada ya pili ya fasihi andishi, mhitimu wa Chuo kikuu cha Mafunzo ya Siasa cha Grenoble na Kituo cha Mafunzo ya Waandishi wa habari jijini Paris.








MAELEZO
Tuma maoni yako kwa makala haya