Pata taarifa kuu
MAREKANI-UE

Barack Obama ziarani Ujerumani

Rais wa Marekani Barack Obama amewasili Jumapili hii katika mji wa Hannover, kaskazini mwa Ujerumani kwa ziara ya siku mbili wakati ambapo anatarajia kukuza pamoja na Kansela wa Ujerumani Angela Markel makubaliano yenye utata ya kibiasharakati ya Umoja wa Ulaya na Marekani.

Rais wa Marekani Barack Obama na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari katika mji wa Hannover, Aprili 24, 2016.
Rais wa Marekani Barack Obama na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari katika mji wa Hannover, Aprili 24, 2016. REUTERS/Wolfgang Rattay
Matangazo ya kibiashara

Katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari katika mji wa Hanover, rais wa Marekani amesema kuwa "Angela (Merkel) na mimi tumekubali ikimaanisha kwamba Marekani na Umoja wa Ualaya wana haja ya kuendeleza mazungumzo ya mkataba wa kiuchumi ujulikanao kama T-TIP. "

Kujadili makubaliano

Kwa kile ambacho ni ziara yake ya tano na ya mwisho nchini Ujerumani kama kiongozi wa Marekani, Barack Obama anafanya ziara yake hiyo kwa "rafiki yake" Angela Merkel, mshirika wake anayemuheshimu zaidi barani Ulaya. Mkutano huu ni hatua ya mwisho ya ziara ya rais wa Marekani ambayo ilimfikisha nchini Saudi Arabia, ili kujaribu kuyahakikishia mataifa ya Ghuba juu ya mshikamano wa msaada zinazopewa na Marekani, kisha Uingereza ili kuionya dhidi ya kujiondoa kutoka Umoja wa Ulaya.

Barack Obama atazindua mapema jioni maonyesho ya viwanda katika mji wa Hannover, viwanda "kutoka" Ujerumani ambapo Marekani ni mshirika wa mwaka huu. Maonyesho haya yanatoa kwa viongozi wa Marekani na Ujerumani mkataba wa kukuza biashara huria kwa sasa uliojadiliwa baina ya Umoja wa Ulaya na Marekani, unaojulikana kama T-TIP Tafta au TAFTA. "Hatutaachana na jitihada zetu kwa kujadili mkataba wa biashara huria pamoja na mshirika wetu mkubwa, soko la Ulaya", pia Barack Obama amevihakikishia vyombo vya habari vya Uingereza. Rais Wa Marekani anataka mkataba huo kabla ya kuondoka mamlakani mwishoni mwa mwaka huu.

Tofauti zaendelea

Mashauriano kuhusu T-TIP hata hivyo mpaka sasa yamekwamat juu ya tofauti zinazoendelea kati ya pande mbili, na kuchochewa na kuongezeka kwa hofu.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.