Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI-MACHAR-SIASA

Sudan Kusini: Machar aapishwa kuwa Makamu wa rais

Kiongozi wa waasi Riek Machar mara tu baada ya kuwasili kwake katika mji mkuu wa Sudan Kusini, Juba, ameapishwa kuwa Makamu wa rais katika serikali ya umoja wa kitaifa.

Kiongozi wa waasi Sudan Kusini, Riek Machar, amepokelewa na wafuasi wake katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Juba, Aprili 26, 2016.
Kiongozi wa waasi Sudan Kusini, Riek Machar, amepokelewa na wafuasi wake katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Juba, Aprili 26, 2016. REUTERS/Jok Solomun
Matangazo ya kibiashara

Machar amewatolea wito raia wa Sudan Kusini kuwa na “umoja” na kuboresha “maridhiano” ili kukomesha mapigano yaliodumu zaidi ya miaka miwili.

“Tunapaswa kuwakusanya raia wetu ili waweze kuungana na kupona majeraha waliokuwa nayo”, ameanza kusema Bw Machar kwa vyombo vya habari katika uwanja wa ndege wa Juba. Machar amepokelewa na mawaziri pamoja na mabalozi aliposhuka ndege.

Aliondoka mara moja na umati wa watu hadi Ikulu ambapo aliapishwa kama Makamu wa rais mbele ya maafisa wa andamizi wa Umoja wa Afrika (AU) pamona na rais wa zamani wa Botswana Festus Mogae, ambaye anaongoza Kamati ya uchunguzi na kutathmini makubaliano ya amani yaliotiliwa saini Agosti 26, 2015.

“Ninajikubalisha kikamilifu kutekeleza makubaliano hayo, ili mchakato wa maridhiano na wa uponyaji uanze pia haraka iwezekanavyo, ili raia waweze kuwa na imani kati nchi ambayo walipigania kwa miaka mingi,” amesema alipokua akiapishwa.

Sudan Kusini, taifa changa duniani, ilijitangazia uhuru wake kati ya mwezi Julai 2011 na mwezi Julai 2013, baada ya miongo kadhaa ya mgogoro pamoja na serikali kuu ya Khartoum.

Riek Machar aliwahi kushikilia wadhifa wa Makamu wa rais kati ya mwezi Julai 2011 na mwezi Julai 2013, wakati ambapo aliachizwa kazi na Rais Salva Kiir. Tangu kutibuka kwa machafuko Disemba 2013, Riek Machar hajarejesha mguu wake katika mji mkuu wa Sudan Kusini, Juba.

Rais Sava Kiir apongeza kurudi kwa Riek Machar

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amekaribisha uamuzi wa Riek Machar kurejea mjini Juba, huku akimtaka kushirikiana kwa ujenzi wa taifa hiclo chana duniani.

"Ninafuraha kubwa kwa kumpokea ndugu yangu Riek Machar (...) na sina shaka kwamba kurejea kwake Juba ni ishara ya mwisho wa vita," Rais Kiir amesema, huku akitoa wito raia wa Sudan Kusini kudumisha amani na kuomba radhi kwa jumuiya ya kimataifa kutokana na kuchelewa kwa mchakato wa amani.

→ Soma zaidi: Riek Machar arejea Juba

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.