Pata taarifa kuu
MAREKANI-UCHAGUZI-SIASA

Kura za mchojo: Trump na Clinton wawabwaga washindani wao

Wakazi wa majimbo matano ya mashariki mwa Marekani wamepiga kura Jumanne hii, Aprili 26 katika kura za mchujo kwa vyama vya Democratic na Republican. Majimbo hayo ni pamoja na Pennsylvania, Maryland, Delaware, Connecticut na Rhode Island.

Donald Trump wakati wa hotuba yake New York, baada ya ushindi wake katika kura za mchujo za "Jumanne Kuu" April 26, 2016.
Donald Trump wakati wa hotuba yake New York, baada ya ushindi wake katika kura za mchujo za "Jumanne Kuu" April 26, 2016. REUTERS/Lucas Jackson
Matangazo ya kibiashara

Donald Trump, kwa upande wa chama cha Republican, amewabwaga washindani wake wote. Upande wa chama cha Democratic, Hillary Clinton ameshinda majimbo manne na kushindwa jimbo moja ambalo mshindane wake Bernie Sanders ameibuka mshindi. Hata kama zoezi hili bado halijamalizika, tayari Donald Trump na Hillary Clinton wanatabiriwa kuwa wagombea urais kwa tiketi ya vyama vyao katika uchaguzi wa urais wa Novemba 8.

Upande wa chama cha Republican, Donald Trump na wafuasi wake wamekuwa wakisherehekea ushindi huo. Bilionea huyo ameshinda majimbo yote matano kwa kuwapiku washindani wake, zaidi ya alama 30 katika majimbo ya Pennsylvania, Maryland na Connecticut.

Kama Donald Trump atakua haijafikia idadi ya wajumbe wanaohitajika kwa ajili ya uteuzi wake kwa tiketi ya chama cha Republican, Ted Cruz na John Kasich watakua hawana tena wasiwasi naye. Na muungano wa wagombea hawa wawili dhidi Trump, uliotangaza wiki hii, unaonekana kuwa hautakua na ushawishi kwenye uchaguzi wa Jumanne hii.

"Ninajiamini tangu sasa kuwa ni mgombea asili", Bw Trump amesema wakati wa hotuba yake ya ushindi, na kuwataka washindani wake kujiondoa katika kinyang'anyiro hicho kwa ajili ya uteuzi wa mgombea urais: "njia bora ya kuuangusha mfumo huo ni kuwa na ushindi kama nilioupata. Ninachukua mfano wa bondia: wakati bondia anambwaga mpinzani wake, huna haja ya kusubiri uamuzi! ", amesema Donald Trump

Majimbo kumi na tano yatapiga kura mwezi Mei na Juni. Donald Trump bado ana uwezo wa kukusanya wajumbe 1,237 kabla ya makubaliano ya Julai. Lakini washindani wake wataendelea kufanya kazi kwa lengo la kumuangusha. Kampeni zitaendelea katika mazingira kama hayo wiki za karibuni.

Ushindi wa Hillary Clinton

Mgombea urais kupitia chama cha Democratic, Hillary Clinton pia ameshinda katika majimbo muhimu. Amembwaga mshindani wake Bernie Sanders katika majimbo ya Maryland, Pennsylvania, Delaware na Connecticut. Hata hivyo, Bernie Sanders, ameibuka msindi katika jimbo la Rhode Island.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.