Pata taarifa kuu
MAREKANI-UCHAGUZI-SIASA

Paul Ryan "bado tayari" kumuunga mkono Trump

Mgogoro unaendelea katika chama cha Republican nchini Marekani, ikisalia miezi sita tu ya uchaguzi wa urais. Paul Ryan anasema bado tayari kumuunga mkono Donald Trump.

Paul Ryan, Mwenyekiti wa Baraza la Wawakilishi kutoka chama cha Republican, Novemba 3, Washington.
Paul Ryan, Mwenyekiti wa Baraza la Wawakilishi kutoka chama cha Republican, Novemba 3, Washington. AFP/AFP/Archives
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Baraza la Wawakilishi na kiongozi wa tatu nchini Marekani amesema hadharani Alhamisi, Mei 5 kwamba anahitaji muda wa kujua mpango wa mgombea urais wa chama cha republican kabla ya kujua kama atampigia kura bilionea huyo, ambaye kwa sasa ni mgombea pekee katika mbio za urais katika chama cha Republican.

Donald Trump yuko katika hatua ya kupata wajumbe wanaohitajika ili aweze kutawazwa kama mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Republican, lakini mgawanyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama hiki kabla ya uteuzi huo.

Paul Ryan, Mwenyekiti wa Baraza la Wawakilishi ameelezea hadharani kutokuridhishwa na hali iliyokikumba chama chao siku ya Alhamisi. "Siniko tayari kuunga mkono sasa hivi, siniko huko bado. Lakini natumaini kufanya hivo, napenda kufanya hivyo. Lakini kile ambacho ni muhimu ni kuunganisha chama. Na nadhani mzigo wa kuunganisha chama unamrudilia "mgombea, ambaye ni Bw Trump, " Paul Ryan amesema.

Kauli ya rais wa Baraza la Wawakilishi, inaonekana imemkera Donald Trump, ambaye, kwa muda mchache baada ya kauli hii ya Bw Ryan, amejibu, akisema: "kauli hii haina umuhimu wowote. Kwa upande wangu, siungi mkono mpango wa Paul Ryan. "

Mgawanyiko huu uliyojitokeza katika chama cha Republican , iwapo utaendelea hadi katika uchaguzi wa urais, unaweza ukampa nguvu mgombea wa chama cha Democratic na kuibuka msindi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.