Pata taarifa kuu
DRC-KATUMBI-SIASA

DRC: Polisi yawatawanya wafuasi wa Katumbi

Polisi imewatawanya Jumatano hii, Mei 11 mamia kwa maelfu ya wakazi wa mji wa Lubumbashi walioambatana na Moïse Katumbi Mahakamani. Mwanasiasa wa upinzani huyo wa upinzani, pia mgombea urais katika uchaguzi ujao wa rais, anasikilizwa kwa mara ya pili na Ofisi ya mashitaka mjini Lubumbashi.

Mpinzani Moïse Katumbi, katika umati wa wafuasi wake, kabla ya kuripoti mbele ya mwendesha mashitaka Mei 9, 2016, Lubumbashi, katika uchunguzi wa madai ya kuajiri askari mamluki kutoka Marekani.
Mpinzani Moïse Katumbi, katika umati wa wafuasi wake, kabla ya kuripoti mbele ya mwendesha mashitaka Mei 9, 2016, Lubumbashi, katika uchunguzi wa madai ya kuajiri askari mamluki kutoka Marekani. © REUTERS/Kenny Katombe TPX IMAGES OF THE DAY
Matangazo ya kibiashara

Moïse Katumbi anashtumiwa kuajiri askari mamluki wa kigeni kwa minajili ya kuzorotesha usalama wa taifa la Congo.

Moïse Katumbi ameripoti asubuhi katika Ofisi ya mashitaka mjini Lubumbashi ambapo askari wengi wametumwa katika eneo hilo.

Bendera ya nchi shingoni mwake, Moïse Katumbi aliambatana na watu wa familia na baadhi ya wapinzani kama Jean-Claude Vuemba Christophe Lutundula, Dany Banza, Jose Endundo na Kyungu wa Kumwanza.

Wafuasi wake ambao pia waliambatana naye walikua wakiimba nyimbo za kumtukuza.

Bw Katumbi aliyetembea kwa mguu hadi Mahakamani, alijitenga na wafuasi wake, muda mchache baadaye, polisi iliwatawanya wafuasi hao kwa kutumia mabomu ya machozi. Baadhi ya wafusai wamekamatwa.

Mkuu wa polisi katika mkoa wa Lubumbashi, Jean Bosco Galenga, ambaye yupo Mahakamani, amelaani utaratibu huo uliotumiwa na polisi, na kuomba askari polisi waliorusha mabomu ya machozi kukamatwa haraka iwezekanavyo.

Wakati huo huo, shughuli zote za kibiashara zimezorota katikati mwa mji wa Lubumbashi. Barabara inayoelekea Mahakamani imefungwa. Watu na magari yamepigwa marufuku kutumia barabara hiyo.

Moïse Katumbi anasikilizwa kwa mara ya pili Jumatano hii. Siku ya Jumatatu, tayari alisikilizwa. Ofisi ya Mashitaka inamuhoji kuhusu madai ya kuajiri askari mamluki. Tuhuma ambazo ametupilia mbali.

Mahakama ya Katiba yatoa msimamo wake

Hayo yakijiri Mahakama ya Katiba nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imesema Joseph Kabila anaweza kubaki katika wadhifa wake baada ya 2016 endapo uchaguzi wa rais hautafanyika mwaka huu (Mahakama ya Katiba)

Mahakama ya Katiba imetoa msimamo huo ikijibu barua iliyowasilishwa na vyama viliyoseikalini, huku matarajio ya kufanyika kwa uchaguzi mwaka 2016 yakisogezwa kila kukicha. Katika uamuzi wake iliyoutoa Jumatano, Mei 11, Mahakama ya Katiba ilisema: "Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila anaweza kubaki katika wadhifa wake baada ya 2016 endapo uchaguzi hautafanyika mwaka huu."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.