Pata taarifa kuu
UFARANSA-JAPAN-G7

Hollande ziarani Japan kwa ajili ya mkutano wa G7

Rais wa Ufaransa, François Hollande, amewasili Alhamisi hii nchini Japan kwa ajili ya mkutano wa G7 utakaofanyika katika mji wa Ise-Shima, kuhusu njia za kuongeza ukuaji wa uchumi duniani na mapambano dhidi ya ugaidi, chanzo kutoka ujumbe wa Ufaransa katika mkutano huo kimesema.

François Hollande azindua Ijumaa ushirikiano wa kipekee na Japan, Tokyo.
François Hollande azindua Ijumaa ushirikiano wa kipekee na Japan, Tokyo. REUTERS/Junko Kimura
Matangazo ya kibiashara

Vipaumbele vya rais wa Ufaransa ni "kuendelea na kasi iliyoanzishwa na mkutano wa COP21 kuhusu mabadiliko ya tabia nchi, kwa hoja juu ya uwazi wa fedha na mapambano dhidi ya ufadhili wa ugaidi ", wasaidizi wa rais Hollande wameliambia shirika la habri la AFP.

Hollande pia anatarajia kukumbusha katika mkutano huu wa kilele, ambao utaendelea hadi Ijumaa, msimamo wa Ufaransa juu ya mikataba ya biashara huria, chanzo hicho kimeongeza.

Rais wa Ufaransa atakayekutana na mwenzake wa Marekani Barack Obama katika mji wa Ise-Shima amesema kwamba anapinga "katika hatua hii" dhidi ya mazungumzo kuhusu TAFTA (au TTIP) ambayo yanaweza kuhitimishwa kati ya Umoja wa Ulaya na Marekani, akikataa " biashara huria bila sheria. "

Ufaransa inatarajia kuomba, hata hivyo, kwa juhudi mpya za G7 katika suala la afya na bei ya dawa.

Katika mpango wake, G7 itajikita Alhamisi hii juu ya "uhifadhi wa urithi wa utamaduni dhidi uvamizi wa kigaidi" baada ya uharibifu wa hazina za Timbuktu, makavazi ya Mosul, mabaki ya mji wa Nimrud au mahekalu ya mji wa Palmyra.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.