Pata taarifa kuu
ZAMBIA

Kiongizi wa kanisa la Aglikan duniani awasili nchini Zambia

Kiongozi wa kanisa la Anglikana duniani mchungaji Rowan Williams amewasili nchini Zambia muda mfupi uliopita ambapo anatarajiwa kuhitimisha ziara yake ya siku 9 barani Afrika akitokea nchini Zimbabwe ambako alikuwa na mazungumzo na rais Robert Mugabe.

Kiongozi wa kanisa la kianglikane, Rowan Williams, jijini  Harare, Octoba 9. 2011.
Kiongozi wa kanisa la kianglikane, Rowan Williams, jijini Harare, Octoba 9. 2011. REUTERS/Philimon Bulawayo
Matangazo ya kibiashara

Wakati wa mazungumzo yake na rais Mugabe, mchungaji Rowan alimataka kiongozi huyo kushughulikia tuhuma zinazoikabili serikali yake kuhusiana na kunyanyaswa kwa baadhi ya waumini wa kanisa hilo nchini humo.

Akiwa nchini Zambia mchungaji Williams anatarajiwa kuwa na mazungumzo na rais wa nchi hiyo Michael Satta ambapo wanatarajia kuzungumzia masuala ya huduma za kijamii nchini humo na baadae kufanya misa maalumu katika kanisa kuu la mjini Lusaka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.