Pata taarifa kuu
DRC

Tume ya Uchaguzi DR Kongo bado yasuasua kutangaza matokeo, Mugabe aitisha uchaguzi

Tume Huru ya Uchaguzi Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo CENI kwa mara nyingine imegwaya kutangaza mshindi wa nafasi ya urais kwa kile ambacho wanasema huenda matokeo hayo yakasababisha kuibuka kwa machafuko.

AFP PHOTO/GWENN DUBOURTHOUMIEU
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inakuja wakati ambapo matokeo ya awali yanaonesha kuwa Rais Joseph Kabila Kabange akiongoza kwa kupata asilimia arobaini na tisa ya kura zote dhidi ya thelathini na tatu za mpinzani wake Etienne Tshisekedi.

CENI imesisitiza matokeo hayo ya mwisho yatatangazwa baadaye hii leo licha ya kuendelea kushuhudiwa mapambano baina ya wapinzani na askari na hapa Reuben Lukumbuka anatueleza hali ilivyo.

Wakati huohuo Rais Mkongwe kuliko wote Barani Afrika ambaye anaongoza nchini ya Zimbabwe Robert Gabriel Mugabe ameitisha uchaguzi wa urais hapo mwakani kumaliza kipindi cha serikali ya umoja iliyoundwa mwaka elfu mbili na nane baada ya ghasia za baada ya uchaguzi.

Rais Mugabe ametoa kauli hiyo wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Chama Tawala cha ZANU-PF uliofanyika huko Bulawayo na kutaka mshikamano katika kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika hapo mwakani.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.