Pata taarifa kuu
TUNISIA

Moncef Marzouki kuapishwa hii leo kuongoza Nchi ya Tunisia

Mwanaharakati na Mkongwe wa Masuala ya Kisiasa nchini Tunisia Moncef Marzouki anatarajiwa kuapishwa kuwa Rais wa kwanza kuchaguliwa tangu kumalizika kwa mapinduzi yaliyoshuhudiwa katika Taifa hilo lililopo Kaskazini mwa Bara la Afrika.

AFP
Matangazo ya kibiashara

Marzouki ambaye ni Mwanaharakati wa Haki za Binadamu na Mpinzani wa zamani amechaguliwa kuwa rais wa kwanza baada ya kuangushwa kwa Utawala Zine Al Abadine Ben Ali kufuatia kutokea kwa mapinduzi ya umma.

Marzouki anatarajiwa kuapishwa baadaye hii leo kuongoza taifa hilo lililopita kwenye wakati mgumu baada ya kutokea kwa machafuko yaliyochochewa na hali ngumu ya maisha na kuchangia kumwagika kwa damu kwenye nchi ya Tunisia.

Baada ya kuchaguliwa kushika wadhifa wa urais Marzouki aliwaambia wanahabari kuwa yupo tayari kuwasaidia wananchi wa taifa hilo kuweza kutimiza ndoto zao ambazo zinaonekana kuanza kupotea.

Marzouki amesema kitendo cha kufanyika kwa mapinduzi nchini Tunisa imekuwa ni ujumbe tosha kwake kujua kile ambacho wananchi wa taifa hilo wanahitaji kutoka kwa viongozi wao kwa maendeleo ya nchi.

Shughuli ya kuapishwa kwa Marzouki itafanyika katika makazi ya Rais ya Carthagendo kinachokuja miezi kumi na moja tangu kuangushwa kwa Zine El Abidine Ben Ali aliyekaa madarakani kwa muda mrefu.

Marzouki amechaguliwa kwa kupata kura mia moja hamsini na tatu kati ya mia mbili na kumi na saba za wanachama wa Mkutano wa Katiba ambao ulikuwa na jukumu la kuchagua Rais wa Taifa hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.