Pata taarifa kuu
ZIMBABWE

Waziri Mkuu wa Zimbabwe Tsvangirai ataka uchaguzi wa rais usogezwe mbele

Waziri Mkuu wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai ametaka serikali ya nchi hiyo kufanya mabadiliko ya kisiasa kwanza kabla ya kuitisha uchaguzi mkuu ambao umependekezwa ufanyike mwakani nchini humo.

Reuters/Philimon Bulawayo
Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu Tsvangirai amesema mabadiliko hayo ndiyo suluhu pekee ya kuhakikisha uchaguzi mkuu utafanyika bila ya uwepo wa matatizo kama ambayo yalishuhudiwa kwenye uchaguzi wa mwisho.

Tsvangirai ametoa kauli hiyo wakati akihutubia mkutano wa mwisho wa Bunge la nchi hiyo na kuanisha ni kweli kabisa serikali ya Umoja imeshindwa kutekeleza masuala mengi ya msingi tangu kuundwa kwake mwaka elfu mbili na nane.

Rais wa Zimbabwe Robert Gabriel Mugabe amependekeza uchaguzi wa urais ufanyike mapema mwakani ili kumaliza kipindi cha serikali ya umoja iliyoundwa baada ya kuibuka kwa machafuko nchini humo.

Tsvangirai amesema miongoni mwa mambo ambayo yanastahili kufanyiwa mabadiliko ni pamoja na katiba ya nchi hiyo hatua ambayo itafanya uchaguzi ujao uwe wa huru na wahaki kwa wananchi wote.

Kauli hii inakuja baada ya Rais Mugabe akiwa kwenye Mkutano Mkuu wa Chama Tawala Cha ZANU-PF kuweka bayana kuwa wanataka uchaguzi wa rais ufanyike hapo mwakani kutamatisha uwepo wa serikali ya umoja.

Tsvangirai amesema Tume ya Usuluhishi nchini Zimbabwe alipendekeza yafanyike mabadiliko ya Katiba katika nchi hiyo ili kuweka usawa wa kisiasa na kuondoa malalamiko ambayo yamekuwa yakitolewa na upinzani kwenye chaguzi.

Serikali ya Umoja iliundwa baada ya uchaguzi wa mwaka elfu mbili na nane uliofuatiwa na machafuko baada ya chama kikuu cha Upinzani za MDC anachotoka Waziri Mkuu Tsvangirai kugomea matokeo ya uchaguzi yaliyompa ushindi Rais Mugabe.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.