Pata taarifa kuu
Zimbabwe-Uchaguzi

Rais Robert Gabriel Mugabe na shutma dhidi ya upinzani

Rais wa Zimbabwe Robert Gabriel Mugabe amewashutumu wapinzani wake kisiasa wanataka kutumia mchakato wa katiba kufanya mapindizu dhidi yake na amewaonya kuwa Chama Cha ZANU-PF kitapinga tishio lolote dhidi ya mustakabali wao.

rais wa Zimbabwe na mpinzani wake Robert Gabriel Mugabe na mpinzani wake ambae pia ni waziri mkuu Morgan Tshvangirai
rais wa Zimbabwe na mpinzani wake Robert Gabriel Mugabe na mpinzani wake ambae pia ni waziri mkuu Morgan Tshvangirai Montage RFI
Matangazo ya kibiashara

Mugabe ambaye anatarajiwa kutimiza umri wa miaka themanini na nane siku ya jumanne amemtuhumu Mpinzani wake Mkubwa Morgan Tsvangrai kutoka Chama Cha MDC kuwa anataka kutekeleza mapinduzi nchini humo.

Rais Mugabe amesema hawatokuwa tayari kuona hilo linatokea na hivyo wamejipanga vyema katika kukabiliana na njama zozote ambazo zinapangwa na upinzani dhidi yake na hata Chama Cha ZANU-PF kinachoongoza serikali ya Umoja kwa ushirikiano na MDC.

Wakati hayo yanajiri Rais wa Zimbabwe Comrade Robert Mugabe ametishia serikali yake kumkataa rais wa Afrika kusini Jackob Zuma kuwa msuluhisihi mkuu wa mgogoro wa kisiasa unaoendelea ndani ya serikali ya muungano.

Rais Mugabe ambaye atatimiza miaka 88 hapo kesho amesema kuwa serikali yake imekwisha mueleza rais Zuma kuhusu uwezekano wa kumkaata kama msimamizi wa yale ambayo yalikubaliwa kwenye mkataba uliotiwa saini kati ya chama cha MDC na ZANU PF kuhusu kugawana madaraka na utekelezaji wa maazimio.

Kauli ya Mugabe imekuja kufuatia kauli ya hivi karibuni ya rais Zuma kukishutumu chama cha ZANU PF kwakutaka kuharakisha na kukiuka baadhi ya maazimio ambayo yako kwenye mkataba kati yake na MDC hali ambayo huenda ikachochea machafuko maoya ya kisiasa nchini humo.

Rais Zuma aliteuliwa na jopo la viongozi toka nchi kumi na tano za SADC ambao walimtaka asimamie mchakato wa utekelezwaji wa maazimio yaliyo kwenye mkataba na hatua ambazo zimechukuliwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.