Pata taarifa kuu
HARARE-ZIMBABWE

Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe awataka wananchi kujenga uchumi wa taifa lao badala ya vurugu za kisiasa

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amewataka wananchi wake kuachana na vurugu za kisiasa na badala yake kuijenga nchi yao ambayo inategemea nguvu kazi kubwa ya vijana. 

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe (kulia) wakati akirejea nyumbani akitokea Singapore alikoenda kwa matibabu
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe (kulia) wakati akirejea nyumbani akitokea Singapore alikoenda kwa matibabu Reuters
Matangazo ya kibiashara

Rais Mugabe ameyasema hayo wakati wa sherehe za kutimiza miaka 32 toka nchi hiyo kujipatia uhuru ambapo pamoja na mambo mengine rais Mugabe ameongelea suala la afya yake.

Kiongozi huyo amesema kuwa alishangazwa na uvumi kuwa Afya yake imeendelea kuzoroka wakati akiwa nchini Singapore amabko alikwenda kwaajili ya kupatiwa matibabu ya kawaida.

Amewataka wananchi kupuuza maneno yakichochezi na badala yake waendelee kuijenga nchi yao ambayo sasa inahitaji juhudi na maarifa kusimamisha uchumi wake.

Rais Mugabe pia ameendelea kusisitiz uchaguzi mkuu kufanyika mwaka huu, huku wachambuzi wa mambo wakidai kuwa endapo rais Mugabe akaondoka madarakani basi chama cha ZANU PF huenda kikafikia tamati.

Nchi hiyo imkubwa na mtikisiko mkubwa wa kisiasa na uchumi kufuatia mvutano unaoendelea kati ya rais Mugabe na waziri mkuu wake Morgan Tsvangirai ambaye anapinga kufanyika mwaka huu kwa uchaguzi mkuu.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.