Pata taarifa kuu
MAREKANI

Rais wa Marekani Obama awaalika Viongozi wanne wa Afrika kuhudhuria mkutano wa G8

Rais wa Marekani Barack Obama ametumwa mwaliko kwa Viongozi wanne kutoka mataifa ya Afrika kuhudhuria Mkutano wa Nchi zenye Utajiri Mkubwa wa Viwanda maarufu kama G8 ambao utafanyika Camp David.

Rais wa Marekani Barack Obama akihutubiwa kwenye moja ya dhifa ambazo zilifanyika Ikulu ya White House
Rais wa Marekani Barack Obama akihutubiwa kwenye moja ya dhifa ambazo zilifanyika Ikulu ya White House REUTERS/Joaquin Sarmiento
Matangazo ya kibiashara

Ikulu ya Marekani inayotambulika zaidi kama White House imethibitisha kutolewa kwa mwaliko huo ambapo Viongozi hao watashirki kwenye mjadala kuhusu usalama wa chakula duniani.

Viongozi ambao wamepata mwaliko huo ni pamoja na Rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Benin Yayi Boni, Rais wa Ghana John Mills pamoja na Waziri Mkuu wa Ethiopia Meles Zenawi.

Taarifa ya Msemaji wa Ikulu ya Marekani imeeleza tayari mwaliko huo umeshafika kwa Viongozi hao ambao watawakilisha nchi nyingine kutoka Barani Afrika kwenye mdahalo huo wa usalama wa chakula.

Viongozi hao wanne watajumuika na Marais kutoka nchi za Ufaransa, Uingereza, Ujerumani, Italia, Canada, Japan, Urusi na Marekani ambao wanaunganisha G8 kwenye mkutano ambao utafanyika tarehe 19 May.

Mkutano huo pamoja na masuala mengine utajikita kuangazia uchumi wa dunia na vikwazo unovipitia pamoja na kuibuka na mbinu mbadala za kuhakikisha changamoto hizo hazijitokezi tena katika siku za usoni.

Mkutano huo wa G8 utarajiwa kujikita kujadili usalama wa chakula kutokana na takwimu zilizotolewa na Umoja wa Mataifa UN kuonsesha ongezeko la bei limezidi kuchupa mipaka kila mara.

Vyakula ambavyo vimekuwa vikikabiliwa na ongezeko la bei ni pamoja na nafaka, mafuta ya mbegu, mchele, maharagwe, nyama na sukari vitu ambavyo vimekuwa vikitumiwa zaidi ya wananchi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.