Pata taarifa kuu

Mwanasheria wa haki za binadamu apinga uteuzi wa mtoto wa rais wa Equatorial Guinea kuwa makamu wa rais

Mwanasheria wa haki za binaadam nchini Ginee ya Ikweta amekosoa hatua ya rais wa nchi hiyo Teodoro Obiang Nguema Basogo ya kumteua mtoto wake kuwa makamu wa Rais.

Teodoro Obiang Nguema, rais wa  Guiné Equatorial.
Teodoro Obiang Nguema, rais wa Guiné Equatorial. Rodrigues Pozzebom/ABr/Wilipédia
Matangazo ya kibiashara

Teodore Obiang ambaye Mali zake zilizoko nchini Marekani zinafanyiwa uchunguzi na anatafutwa na Ufaransa kwa makosa ya kutapakanya pesa kwa anasa aliapishwa siku ya jumatatu.

Hatua ya Rais huyo kumteua mtoto wake kuwa makamu wa Rais ni hila ya kiongozi huyo kumuandaa mwanaye kuwa Rais hapo baadae, mkurugenzi mtendaji wa shirika linalotetea haki za binaadam, Tutu Alicante ameeleza.

Imeelezwa kuwa Obiang aliongeza mishahara ya wanajeshi mara mbili zaidi bila kuidhinishwa na Bunge hilo, ili kuutetea uamuzi wa uteuzi wa mtoto wake.

waendesha mashtaka nchini Ufaransa umetoa wito wa kutolewa waranti ya kukamatwa kwa Obiang ili kuhojiwa katika uchunguzi wa vyanzo vya pesa zilizotumiwa nchini Ufaransa na Obiang, rais wa Congo Brazaville Denis Sassou Nguesso na aliyekuwa Rais wa Gabon,marehemu Omar Bongo Ondimba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.