Pata taarifa kuu
Zimbabwe

Mugabe asema yuko tayari kukabidhi madaraka akishindwa uchaguzi

Rais Mkongwe wa Zimbabwe Robert Gabriel Mugabe ametangaza utayari wake wa kukabidhi madaraka kwa mshindi wa uchaguzi wa urais ambao utafanyika nchini humo na kuwa kikomo cha serikali ya Umoja wa Kitaifa endapo yeye atashindwa. 

Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai ndiye ambaye ametoa kauli hiyo kuthibitisha utayari wa Rais Mugabe kuwa tayari kuachia madaraka iwapo ataanguka kwenye uchaguzi wa Rais.

Uchaguzi huo ambao umepangwa kufanyika miezi kumi na miwili ijayo unatarajiwa kuwa ni kinyang'anyiro kikali baina ya Rais Mugabe na Waziri Mkuu Tsvangirai ambao kwa sasa vyama vya vya ZANU-PF na MDC zimeunda serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Tsvangirai akiwa ziarani nchini New Zealand ameweka bayana kuna kila dalili kwa Rais Mugabe kukubaliana na matokeo ya uchaguzi ujao iwapo ataangiushwa ni wazi kabisa atakaa kando kumpisha mshindi wa uchaguzi huo.

Waziri Mkuu Tsvangirai akaenda mbali zaidi na kuongeza hakuna sababu itakayomsukuma Rais Mugabe awe chanzo cha nchi hiyo kuingia kwenye machafuko kama yale ambayo yameshuhudiwa mwaka elfu mbili na nane.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.