Pata taarifa kuu
ZAMBIA-CHINA

Serikali ya Zambia yawahakikishia usalama wawekezaji raia wa China walioko nchini humo

Serikali ya Zambia inayoongozwa na Rais Micahel Sata imelazimika kutoa hakikisho la usalama kwa wawekezaji wa kigeni ikiwa ni siku kadhaa baada ya kutokea kwa kifo cha Mkuu wa Migodi ya Madini inayomilikiwa na Kampuni ya China. 

Rais wa Zambia, Michael Sata akiwa na balozi wa China nchini humo, Zhou Yuxiao
Rais wa Zambia, Michael Sata akiwa na balozi wa China nchini humo, Zhou Yuxiao Reuters
Matangazo ya kibiashara

Serikali imesema licha ya kifo cha Wu Shengzai kilichosababisha na kupigwa na wafanyakazi lakini wao wamejipanga vyema kabisa kutoa ulinzi wa uhakika kwa wawekezaji ili watekeleze majukumu yao bila hofu.

Msemaji wa Serikali Kennedy Sakeni amesema Jamii yote ya Wachina haitakiwi kuwa na mashaka yoyote na watapatiwa ulinzi wa kutosha kwa kuwa wamekwenda kuwekeza katika Taifa lao.

Polisi nchini humo tayari wameanzisha uchunguzi kuhusiana na tukio la kuuawa kwa mkuu huyo wa mgodi wa shaba ambaye alishambuliwa na wananchi wenye hasira waliodai kuwa amekuwa akiwanyanyasa.

Serikali ya China iliiandikia barua serikali ya Zambia kueleza kusikitishwa kwake na tukio hilo na kuhoji usalama wa wananchi wake ambao wanamakampuni ya uchimbaji madini nchini humo ambo kwasasa usalama wao uko hatarini.

Serikali ya China pia ilitaka kuhakikishiwa usalama wa wafanyakazi wake wengine ambao wako nchini Zambia kwa shughuli nyingine mbali uwekezaji kwenye sekta ya madini.

Nchi ya China inaongoza kwa kuwa na makampuni mengi ya uwekezaji barani Afrika lakini kampuni hizo zimejikuta matatizoni kutokana na wananchi wengi kukosoa jinsi ambavyo wamiliki wa makampuni kutoka China yanavyowatendea wazawa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.