Pata taarifa kuu
Zimbabwe

Rais Zuma nchini Zimbabwe kushinikiza mabadiliko ya kisiasa

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma yuko nchini Zimbabwe anakojadiliana na viongozi wa kisiasa nchini humo kushinikiza mabadiliko kabla ya uchaguzi mkuu mwaka ujao.

Matangazo ya kibiashara

Rais Zuma ambaye ni mpatanishi wa mzozo wa siasa za Zimbabwe kupitia Muungano wa nchi za Kusini mwa Afrika SADC,  pia anatarajiwa kuwashinikiza viongozi wa kisiasa nchini humo kuharakisha mabadiliko hayo ikiwemo upatikanaji wa katiba mpya.

Tangu mwaka 2009 Zimbabwe imekuwa ikiongozwa na serikali ya muungano baada ya machafuko ya baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2008, uchaguzi ambao kiongozi wa upinzani Morgan Tsvangirai alidai kuibiwa kura na rais Mugabe.

Wawakilishi wa Waziri Mkuu Morgan Tsvangirai wa chama cha MDC,  na rais Robert Mugabe wa chama cha ZANU-PF tayari wamemaliza mchakato wa kuandaa rasimu ya katiba mpya inayaotarajiwa kupigiwa kura mwaka huu.

Jumuiya ya Kimataifa ikiongozwa na Marekani pia imekuwa ikishinikiza Zimbabwe kuhakikisha kuwa kura ya maoni kuhusu katiba mpya inafanyika  kwa haraka kabla ya Uchaguzi Mkuu,huku ikiahidi kuiondolea vikwazo.

Rais Mugabe ambaye ameongoza nchi hiyo kwa miaka 32 iliyopita, amenukuliwa akisema  atawania tena urais mwakani.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.