Pata taarifa kuu
ZIMBABWE

Rais Mugabe atangaza siku za kupigia kura rasimu ya katiba na siku ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa Urais

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ametangaza tarehe ambayo wananchi wa taifa hilo watapigia kura rasimu ya mabadiliko ya katiba mpya pamoja na siku ambayo nchi hiyo itafanya uchaguzi mkuu.

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe (kulia) akiwa na waziri mkuu wake Morgan Tsvangirai (kushoto)
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe (kulia) akiwa na waziri mkuu wake Morgan Tsvangirai (kushoto) Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kwenye barua aliyoiandikia mahakama kuu mjini Harare rais Mugabe amependekeza muda wa kupigia kura rasimu ya katiba uwe mwezi wa kumi na moja mwaka huu na siku ya kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu iwe mwezi wa tatu.

Hatua ya rais Mugabe imeelezwa kama njia moja wapo ya kiongozi huyo kutaka kuinusuru nchi hiyo kutumbukia kwenye matatizo mengine ya kisiasa mara baada ya vurugu za uchaguzi za mwaka 2008.

Kumekuwa na mvutano kati ya rais Mugabe na waziri mkuu wake Morgan Tsvangirai kuhusu tarehe ya uchaguzi mkuu pamoja na kupigia kura rasimu ya mabadiliko ya katiba mpya.

Serikali ya umoja wa kitaifa nchini Zimbabwe iliundwa mwaka 2008 na toka kipindi hiko kumekuwa na shinikizo la kutakiwa kufanyika mabadiliko ya katiba ya nchi hiyo sula ambalo sasa huenda likatimia.

Rais Mugabe anataka wiki ya mwanzo wa mwezi wa kumi na moja ndio iwe wiki ambayo wananchi watapiga kura kuhusu rasimu ya mabadiliko ya katiba kabla ya kuelekea kwenye maandalizi ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo.

Chama tawala nchini humo cha ZANU-PF kimepinga mapendekezo mengi ya kwenye katiba ya nchi hiyo na kutaka uchaguzi mkuu ufanyike hata kama matokeo ya kura ya rasimu ya katiba mpya yataamua vinginevyo.

Chama hicho kimekuwa kikikosolewa na wanasiasa wa upinzani pamoja na wanaharakati wa kutetea haki za binadamu kwa kutaka kuweka kizuizi cha kupatikana kwa katiba mpya ya nchi ambayo itapelekea kuwepo kwa uchaguzi ulio huru na haki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.