Pata taarifa kuu
TUNISIA

Polisi nchini Tunisia watumia risasi za mpira kutawanya waandamanaji Sidi Bouzid

Jeshi la polisi nchini Tunisia limetumia risasi za mpira na mabomu ya machozi kuwasambaratisha mamia ya waandamanji huko Sidi Bouzid ambo walikuwa wakidai kujiuzulu kwa gavana wa jimbo hilo.

Waandamanaji wakiwa katika moja ya mikusanyiko yao nchini Tunisia
Waandamanaji wakiwa katika moja ya mikusanyiko yao nchini Tunisia maishani.blogspot.com
Matangazo ya kibiashara

Takribani waandamanaji elfu moja walijikusanya katikati ya mji mkuu wa Tunisia eneo lililozaliwa harakati zilizomwondoa madarakani mtawala wa zamani Zine El Abidine Ben Ali hapo mwaka jana,lakini sasa tuhuma zimeelekezwa kwa gavana kutofaa na kutakiwa kujiondoa madarakani.

Baadhi ya waandamanaji walijaribu kuvamia makao makuu ya jimbo hilo ambapo walikumbana na ulinzi mkali wa polisi na majeshi ambapo risasi za tahadhari zilirushwa ili kuwazuia waandamanaji hao kukaribia maeneo hayo.

Taarifa zinabainisha kuwa jeshi la polisi liliwahi kumwokoa gavana huyo kwa kumuondoa ofisini mwake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.