Pata taarifa kuu
BAHRAIN

Serikali nchini Bahrain yapiga maruku maandamano na mikusanyiko kukabiliana na machafuko ya Washia na Wasunni

Serikali ya Bahrain imetangaza kupiga marufuku maandamano ya aina yoyote na mikusanyiko kwa lengo la kuimarisha usalama katika nchi hiyo tamko linalokuja baada ya kutokea machafuko kati ya Washia na Vikosi vya Ulinzi katika nchi hiyo inayotawaliwa Kisunni.

Serikali nchini Bahrain imepiga marufuku maandamano na mikusanyiko yote ambayo imekuwa ikiandaliwa ili kuimarisha hali ya usalama
Serikali nchini Bahrain imepiga marufuku maandamano na mikusanyiko yote ambayo imekuwa ikiandaliwa ili kuimarisha hali ya usalama Reuters
Matangazo ya kibiashara

Tangazo hilo limetolewa kupitia taarifa iliyotolewa na Sheikh Rashind Bin Abdullah Al Khalifa na kutolewa na Shirika la Utangazaji wa nchi hiyo BNA na limeweka bayana uammuzi huo umechukuliwa mahsusi kwa ajili ya kulinda amani ya raia.

Taarifa hiyo imesema kutokana na kuendelea kwa machafuko ya kila uchao nchini Bahrain baina ya waumini wa Shia na wale wa Sunni wameona njia pekee ya kurejesha usalama wa kudumu ni kwa kupiga marufuku mikusanyiko na maandamano ya aina yoyote.

Serikali ya Bahrain imesema mikusanyiko yoyote haramu na maandamano ambayo yataandaliwa bila kufuata sheria yatakutana na mkono wa sheria huku wahusika watakaokamatwa watakuwa na kesi ya kujibu.

Waziri Sheikh Abdullah Al Khalifa amesema wanaendelea pia kukifuatilia kikundi cha Washia kinachotambulika kwa jina la Al Wefaq ambacho kinaaminika kupanga njama za kutaka kutatiza shughuli za serikali.

Serikali ya Bahrain pia imekataa ombi la Kundi la Al Wafeq ambalo lilitaka kufanya maandamano siku ya jumapili katika Kijiji cha Akar ambacho kipo karibu na Manama wakisema wanahofia hali ya usalama.

Kijiji cha Akar kilishuhudia askari mmoja akijeruhiwa na bomu katika ghasia ambazo zilitokea tarehe 18 ya mwezi Oktoba kitu ambacho kinaongeza hofu zaidi ya kiusalama na hata kupigwa marufuku kwa maandamano.

Viongozi wa Kishia nchini Bahrain wamekuwa wakikabiliwa na ukosaji mkubwa kutokana na kile ambacho kinaelezwa ni wao kukiuka haki za binadamu na hivyo kutekeleza ukatili dhidi ya Washia.

Takwimu zinaonesha kuwa tangu tarehe 14 february 2011ambapo nchi ya Bahrain ilishuhudia kuanza kwa maandamano watu thelamini wamepoteza maisha na serikali ikisema jumla ya askari 1500 wamejeruhiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.