Pata taarifa kuu
ZIMBABWE

Matokeo ya mwisho ya kura ya maoni kuhusu Katiba mpya nchini Zimbabwe kutangazwa siku ya Jumanne

Matokeo ya mwisho ya kura ya maoni kuhusu rasimu ya Katiba mpya nchini Zimbabwe inatarajiwa kutolewa siku ya Jumanne.

Matangazo ya kibiashara

Tume ya uchaguzi nchini humo inasema itatoa matangazo hayo mchana ili kumaliza zoezi hilo lililoanza siku ya Jumamosi juma lililopita.

Hesabu iliyofanywa na kundi la Waziri Mkuu Morgan Tsvangirai inaonesha kuwa zaidi ya asilimia tisini ya wananchi nchini humo wamepiga kura ya ndio na dalili zote zinaonesha kuwa rasimu hiyo imeungwa mkono kikamilifu.

Uwepo wa katiba mpya nchini humo utawezesha kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu mpya ambao utaamua ikiwa rais wa sasa Robert Mugabe atawania urais nchini humo au la.

Katiba mpya inaweka muda wa mihula miwili kwa rais kutawala nchi hiyo na inaipa bunge nguvu zaidi ya kuidhinisha uteuzi uliofanywa na rais.

Ikiwa Robert Mugabe mwenye umri wa miaka 89 atawania tena urais nchini humo ataweka historia kuwa kiongozi mkongwe zaidi barani Afrika kuwania urais.

Rais Mugabe ambaye amekuwa rais tangu mwaka 1980 pia ameunga mkono katiba hiyo mpya, na ikiwa atachaguliwa kwa mihula miwili ataongoza nchi hiyo kwa miaka kumi ijayo.

Waangalizi wa kutoka muungano wa mataifa ya Kusini mwa Afrika SADC wamesema zoezi hilo la kura la maoni limefanyika kwa amani licha ya visa vichache vya machafuko.

Uchaguzi Mkuu nchini Zimbabwe unatarajiwa kufanyika mwezi Julai mwaka huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.