Pata taarifa kuu
ZIMBABWE

Wabunge nchini Zimbabwe kufanya mjadala wa kupitisha muswada wa Sheria ya Katiba Mpya itakayotumika kwenye Uchaguzi Mkuu

Bunge nchini Zimbabwe linatarajiwa kuanza mchakato wa kupitisha mswada wa sheria mpya ulioidhinishwa kwa kura ya maoni iliyopigwa na wananchi wa Taifa hilo mwezi March mwaka huu. Wabunge wataanza kibarua hicho juma lijalo kwa kupitisha muswada huo kabla ya Baraza la Seneti halijafanyakazi ya mwisho na hatimaye taifa la Zimbabwe liweze kupata katiba mpya itakayomaliza muda wa ile iliyoanza kutumika tarehe 18 mwezi April 1980.

Waziri Mkuu wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai akiwa Bungeni ambako kunatarajiwa kutumika kupitisha muswada wa katiba mpya
Waziri Mkuu wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai akiwa Bungeni ambako kunatarajiwa kutumika kupitisha muswada wa katiba mpya
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Katiba Eric Matinenga amethibitisha kuanza kwa mjadala mkali juma lijalo katika Bunge nchini Zimbabwe ambapo wabunge wapatao theluthi mbili wakiridhia itatambulika kama katiba mpya.

Wabunge wanaofika theluthi mbili wakishapitisha ndiyo kazi itabaki kwa Rais Robert Mugabe kusaini ili iwe sharia mpya na hivyo Zimbabwe itakuwa imepata katiba itakayotumika kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Katiba hiyo Mpya inaweza ikawa kikwazo kwa viongozi wenye uroho wa madaraka kwa kuwa inatoa kipindi cha mihula miwili pekee kwa yule atakayechaguliwa kuwa Rais badala ya ilivyo sasa ambapo Rais Mugabe amekuwa madarakani tangu uhuru.

Katiba hiyo mpya pia ikipitishwa itaondoa kinga ya Rais pindi akiondoka madarakani na hivyo ataweza kushtakiwa kwa makosa ambayo ameyafanya akiwa madarakani huku ikiongeza nguvu ya Mahakama.

Wananchi wa Zimbabwe wanaweza wakanufaika na katiba hiyo mpya ambayo inasimamia amani na maridhiano sambamba na kusaka suluhu ya machafuko yote yanayozuka baada ya kufanyika kwa uchaguzi mkuuu.

Katiba mpya ya Zimbabwe ilikuwa inapiganiwa zaidi na Chama cha Upinzani cha MDC kinachoongozwa na Waziri Mkuu Morgan Tsvangirai ambaye amekuwa akilalamikia kuibiwa kura zake kila uchaguzi unapokamilika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.